• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

Elimu ya sekondari

Mr. Martoni James

CHEO

MAWASILIANO


Kaimu Afisaelimu Sekondari

+255 764 719 498/ 0784647 183 

elimusekondary@ngaradc.go.tz

TAARIFA YA MAENDELEO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI

Utanguliza:

Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ina jumla ya shule 29, kati ya hizo 23 ni za serikali na 6 ni za binafsi.  Aidha miongoni mwa hizo kuna shule 5 za kidato cha tano na sita zikiwemo 4 za serikali na 1 ni ya binafsi hivyo kutimiza azima ya Serikali ya kila tarafa kuwa na shule ya kidato cha tano na sita. Halmashauri ya Wilaya ina jumla ya walimu 470 kati ya hao walimu wanaofundisha masomo ya sanaa ni 395 na wanaofundisha masomo ya hisabati na sayansi ni 75.  Jukumu kubwa la idara ya Elimu Sekondari ni kuhakikisha kuwa vijana wote wanaojiunga na masomo ya Sekondari wanahitimu na kufaulu kwenye mitihani yao ya mwisho.

UTEKELEZA WA MIRADI KWA MWAKA 2017/2018

Halmashauri ya wilaya kupitia idara ya Elimu Sekondari kwa mwaka ulioishia Juni 2018 ilitekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya bweni moja lenye thamani ya Tsh.191,618,752.16 lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 112 katika shule ya sekondari Muyenzi kwa ufadhili wa Mamlaka ya elimu Tanzania (TEA). Vilevile Halmashauri inaendelea kutekeleza miradi ya ujenzi wa madarasa 4 katika shule za Rusumo B darasa 1, Ngara 1 na Nyamiaga madara 2 na kukamilisha maabara 22 za sayansi katika shule za Shunga,Rusumo,Kanazi, Kibimba,Ndomba, Mugoma na Bukiriro kwa Tsh.212,042,140.94 chini ya ufadhili wa Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R).

USAJILI WA WANAFUNZI MWAKA 2018

Usajili wa wanafunzi wa kidato cha kwanza waka 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ilipangiwa wanafunzi kidato cha kwanza 3813 kwa mwaka 2018 ikiwa sawa na asilimia 100 ya wanafunzi wote 3813 waliohitimu darasa la saba kwa mwaka 2018 kujiunga na shule za kutwa. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa, walioripoti ni wanafunzi 3564 Sawa na 93%.

Usajili wa wanafunzi wa kidato cha tano mwaka 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ilipangiwa na OR-TAMISEMI wanafunzi kidato cha tano 839 kwa mwaka 2018. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa, walioripoti ni wanafunzi 664 Sawa na 79% hadi sasa.

MAFANIKIO

Kuna baadhi ya mafanikio tuliyofikia;

  1. Ufaulu wa wanafunzi kwa mtihani wa Taifa wa kidato cha nne na sita kuongezeka kwa  kipindi cha miaka mitatu.
  2. Kata zote zina shule za sekondari isipokuwa kata ya Nyamagoma ambayo ni kata mpya.
  3. Kila Tarafa ina shule ya kidato cha tano na cha sita.
  4. Kila shule kujifunza masomo ya sayansi kwa vitendo kutokana na upatikanaji wa vifaa na madawa ya maabara yanayotokana na fedha ya ruzuku ya uendeshaji.
  5. Kukamilisha maabara 46 kati ya maabara 72 zinazohitajika wilaya nzima ambazo ni sawa na asilimia 64.

CHANGAMOTO 

Pamoja na mafakio tajwa Idara ya Elimu Sekondari inaendelea kukabiliana na changamoto kadhaa;

  1. Utoro wa reja reja kwa baadhi ya wanafunzi ambao huathiri ujifunzaji.
  2. Umbali mrefu wa makazi ya wanafunzi na walimu kutoka/kwenda shuleni.
  3. Baadhi ya wanafunzi wanaishi katika mazingira yanayoathiri ujifunzaji wao.
  4. Upungufu mkubwa wa walimu wa Hisabati na  Sayansi
  5. Upungufu wa miundombinu ya nyumba za walimu,vyoo vya wanafunzi, vyumba vya madarasa na majengo ya utawala.

Mikakati ya Kuboresha Taaluma

Baadhi ya mikakati ya kuboresha ufaulu wa wanafunzi katika mwaka 2018;

  1. Wakuu wa shule na walimu wameelekezwa kudhibiti utoro wa reja reja kwa wanafunzi kwa kusimamia mahudhurio ya wanafunzi na kutoa ushauri nasihi.
  2. Idara ya Elimu Sekondari kwa kushirikiana na Wathibiti Ubora wa Elimu wa wilaya wanafanya ufuatiliaji wa mara kwa mara shuleni.
  3. Kujenga daharia/hostel katika shule za kutwa kwa kuishirikisha na kuihamasisha jamii kuona umuhimu wa daharia hizo.
  4. Kuweka kambi za masomo kwa madarasa ya mitihani ya Taifa Mitihani inapokaribia kufanyika.
  5. Wakuu wa shule na walimu wa taaluma wanahimizwa kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya Afisaelimu Mkoa ya kutoa mazoezi yenye ubora kila siku za masomo hasa kwa wanafunzi wa kidato cha II na cha IV.
  6. Kufanya mitihani ya utimilifu (Mock) ya Wilaya na Mkoa pamoja na mitihanin ya ujirani mwema.

Taarifa maendeleo elimu sekondari.pdf

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2019 January 09, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2019 January 09, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2019 January 09, 2020
  • Matokeo ya mitihani iliyofanyika 2017 January 30, 2018
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • ZIARA YA MKUU WA WILAYA NA MKURUGENZI MTENDAJI KUTEMBELEA UJENZI WA MADARASA KWA AJILI YA MAPOKEZI YA KIDATO CHA KWANZA 2021

    January 05, 2021
  • MKURUGENZI AWAAGIZA VIONGOZI WA KATA MPAKA VITONGOJI KUHIMIZA MATUMIZI BORA YA VYOO NA USAFI WA MAZINGIRA

    August 12, 2020
  • NGARA YAGEUKA KIVUTIO KWA WENGI MAONESHO YA NANENANE 2020

    August 08, 2020
  • MKUU WA WILAYA NGARA AWASIFU WAKULIMA WA NGARA

    August 07, 2020
  • Tazama zote

Video

Moto Rusumo Agosti 2018
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa