- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kwa kipindi cha karibuni nchi mbalimbali duniani zimeendelea kutoa taarifa za uwepo wa visa na vifo kutokana na magonjwa mbalimbali ya mlipuko. Baadhi za dalili za magonjwa zilizotolewa taarifa zinazojumuisha:
Kwa kuzingatia uwepo wa taarifa hizo, Serikali imeendelea kuimarisha ufuatiliaji wa viashiria na tetesi za uwepo wa dalili za magonjwa ya mlipuko. Hadi sasa kuna tetesi zimeripotiwa kwa Mkoa wa Kagera na Serikali imechukua hatua kadhaa za haraka ikiwemo: kuleta timu ya wataalamu; kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hili; kuchukua sampuli na kufanya vipimo vya maabara.
Wakati hatua nyingine zinaendelea; Timu ya Dharura ya Mkoa, tunatoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano kwa kuzingatia kanuni za afya ikiwemo kuchukua tahadhari zifuatavyo:
Serikali imejipanga kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora, sahihi na kwa wakati.
Hivyo endapo utaona mtu mwenye mojawapo ya dalili zilizotajwa toa taarifa haraka kwa kituo cha huduma za afya kilicho karibu, ofisi ya serikali ya kijiji/mtaa/kata au piga simu 199 bila malipo au 0774 442 389.
Kwa msingi huo, Serikali inawahimiza wananchi wote kutoa ushirikiano ili kulinda afya ya jamii yetu. Tukumbuke, kinga ni bora kuliko tiba.
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa