- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wednesday 29th, January 2025
@Uwanja wa posta ya zamani Ngara mjini.
Bonanza la Itambue Afya yako 2023 lililofadhiliwa na Radio Kwizera (Mfadhili Mkuu),wakishirikiana na Halmashauri Idara ya Afya wilaya ya Ngara, Tembo Nikel, NMB,CRDB, Nyamiaga food production, Hotel za Free Park, Amahoro B na A, Alfa Hotel na Mbunge Jimbo la Ngara Mhe Ndaisaba G.Ruholo limefanyika leo March 18/2023 katika Viwanja vya Posta ya Zamani Mjini Ngara mkoani Kagera
Katika Bonanza hilo Mashabiki Wanawake wa kipindi cha Asubuhi Njema cha Radio Kwizera wameibuka Mabingwa katika soka kwa kushinda magoli 2-0 dhidi ya Mashabiki Wanawake wa kipindi cha Mchakato huku kwenye kuvuta Kamba pia Asubuhi Njema wakiwafunga Mchakato kwa mizunguko yote minne.
Kwa ushindi huo asubuhi njema wamekabidhiwa zawadi ya fedha Laki 4 na Afisa Michezo wilaya ya Ngara Said Salum aliyekua mgeni rasmi huku Mchakato wakipata shilingi Laki 2 na elfu 25.
Michezo iliyoshindawa ni soka wanawake, kufukuza kuku, Kuvuta kamba na kukimbia kwenye Magunia.
Washindi wa michezo kuanzia 1 Hadi 3 wamepatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu.
Aidha kumefanyika zoezi la uchangiaji damu , upimaji wa afya Magonjwa mbalimbali imefanyika uwanjani hapo zaidi ya watu 495 wampima afya zao na kupata ushauri wa kitaalam.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa