• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

MAADHIMISHO YA KILELE CHA KAMPENI YA "USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO"-NGARA

Friday 9th, May 2025
@KATA YA MUGOMA,NGARA

Katika maadhimisho ya kilele cha kampeni ya Nyumba ni Choo wilayani Ngara iliyofanyika katika kata ya Mugoma  siku ya Jumatano,05/06/2019,Mhamasishaji mkuu Mrisho Mpoto aliwaeleza wananchi wa Mugoma juu ya faida za matumizi bora ya choo kilicho bora au cha kisasa.

    Mhamasishaji Mrisho Mpoto

Mrisho Mpotoo alisema,”Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inawataka watu wawe na choo Bora au kama una uwezo ujenge choo cha kisasa.Serikali inawakumbusha kuwa choo bora ni kile chenye kuta nne imara, kilichoezekwa juu kwa bati au nyasi kulingana na uwezo wa mwananchi kwa ajili ya kuzuia mvua kujaza shimo la choo.Pia choo bora lazima kiwe na mlango unaofunga ili kuwa na faragha kwa mtumiaji pamoja na kuzuia wadudu walukao na kutambaa wanaoweza kueneza magonjwa na kuhatarisha afya zetu.Mwisho choo bora kinatakiwa  kuwa na mfuniko wa kufunikia tundu la choo pamoja na kuwa na sakafu inayoweza kusafishika pamoja na pomba la kutolea hewa chafu.”

Pia Mrisho Mpoto alitoa elimu ya hatua sahihi za unawaji mikono kabla ya kula na baada ya kutoka chooni. Elimu hii aliitoa kwa vitendo ambapo wanafunzi walionesha kwa matendo hatua hizo mbele ya hadhara yote iliyokuwa imekusanyika.

Baada ya Mrisho Mpoto kutoa elimu juu ya kampeni ya usichukulie poa nyumba ni choo, Afisa Afya wa Wilaya ya Ngara Ndugu Salumu Kimbau alitoa ripoti ya Wilaya ambapo alisema ni asilimia 33.2 tu wanachi wa Ngara ambao wana vyoo bora na asilimia 66.8 ikiwa na vyoo visivyo bora.

     Afisa Afya Ngara, Ndugu Salumu Kimbau

Pia alieleza changamoto zinaikumba idara ya Afya wilayani ngara ikiwemo; uchache wa wataalam wa Afya pamoja na uchache wa Vyombo vya usafiri ambavyo huwawea vigumu wao kutimiza majukumu yao kwa uharaka kama kutoa elimu na uhamasishaji pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara katika vijiji vya wilayani Ngara.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan J. Bahama alitoa shukrani zake za dhati kwa tume ya uhamasishaji wa Usichukulie poa nyumba ni choo kwa kuwakumbusha wanachi juu ya umuhimu wa kujenga na kutumia vyoo bora. Pia aliwaasa wanachi wote wilayani Ngara kuanza kujenga vyoo bora maana ni asilimia 33.2 tu katika hii  ambao wana vyoo vilivyo bora ili kufikia mwishoni mwa mwaka 2019, Ngara iwe na vyoo bora kwa asilimia 99 mpa 100.

   Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngara, Ngugu Aidan Bahama J. Bahama

Mkurugenzi wa Wilaya alielezea pia changamoto zilizopelekea Wilaya ya Ngara kuwa na asilimia chache za watu wenye vyoo bora ikiwemo; Uwepo mdogo wa wafanyakazi wa Afya kuanzia ngazi ya Kijiji mpaka Wilaya pia uwepo wa wazee na watu wasiojiweza ambao imewawea ngumu kuwa na vyoo bora vinavyotakiwa na serikali.

“Changamoto hizi huweza kutatuliwa kama hawa wafanyakazi wachache wataweza kuweka nia ya kuwaelimisha wananchi kuwa sasa ni zama za kuwa na vyoo bora na si bora choo.”Alisema Mkurugenzi.

 Pia Mkurugenzi aliwaomba watendaji wa Vijiji kushirikiana na wananchi kaya kwa kaya na kuhakikisha kila kaya inatumia choo kilicho bora.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ngara Ruten Kanali Michael  M. Mntenjele alionesha kusikitishwa na asilimia kubwa ya wanachi wa Wilaya ya Ngara kutokuwa na vyoo bora. Aliwaomba Waheshima madiwani kuhakikisha wanashughulikia kaya ambazo hazina vyoo kabisa kuweza kujenga vyoo bora ndani ya muda mfupi ujao. Pia alitoa ahadi ya kuwa na vyoo bora wilayani Ngara kwa wananchi wake wote ndani ya muda mfupi kabla ya mwaka 2019 kuisha.

  Mkuu wa Wilaya Ngara, Lt Col Michael M. Mntenjele

Pia Mkuu wa Wilaya aliwaasa wanachi akisema “kuzingatia matumizi ya choo bora ni wajibu wa kila mwanachi pamoja na kujenga vyoo bora kwa manufaa ya Afya ya kila mmoja wetu”.

Sherehe za maadhimisho haya ziliambatana na burudani mbalimbali kutoka kwa vikundi vya Ngoma,kucheza na nyoka pamoja na michezo ya sarakasi iliyovutia macho ya wananchi  wengi.



Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI ROBO YA TATU 2024/2025 WAFANYIKA UKUMBI WA COMMUNITY CENTRE NGARA MJINI

    May 07, 2025
  • MKUU WA MKOA MHE HAJAT FATMA ABUBAKARI MWASSA AENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDEKEO WILAYA YA NGARA

    May 03, 2025
  • MHE HAJJAT FATMA MWASSA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO WILAYA YA NGARA

    May 02, 2025
  • MKUU WA MKOA MHE HAJAT FATMA MWASSA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA WAFANYAKAZI ZAFANA KIMKOA WILAYA YA NGARA

    May 01, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa