• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

Health Services

Idara ya Afya imeendelea kutoa huduma za Afya kwa wananchi kupitia vituo vya huduma 61 ambavyo ni Hospitali 3 Vituo vya Afya 5 na Zahanati 53.  Kati ya hivyo vituo vinavyo milikiwa na serikali ni hospital 1, Vituo vya afya 4 na zahanati 45. Huduma zimeendelea kutolewa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama MDH, SAPO, MARIA STOPES, JHPIEGO USAID-B0RESHA AFYA, Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Kagera, Kanisa la katoliki Dayosisi ya Rulenge Ngara, PSI na Shirika la ABT ASSOCIATES. 

UTEKELEZAJI WA HUDUMA ZA AFYA

  • Idara imeendelea kutoa huduma zake katika vituo vyake kupitia vipaumbele vilivyowekwa na Wizara ya Afya ambavyo ni:
  • Kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.
  • Kuboresha huduma ya Afya ya uzazi na mtoto
  • Kuzuia na kutibu magonjwa ya kuambukiza.
  • Kutibu magonjwa ya siyo ya kuambukiza.
  • Tiba na huduma za magonjwa yasiyopewa kipaumbele katika Jamii.
  • Kuboresha Huduma za Usitaw iwa Jamii
  • Kuimarisha ujenzi, ukarabati wa miundo mbinu katika sekta ya Vituo vya huduma za afya.

UPATIKANAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA

Dawa katika vituo vya kutolea huduma za Afya zinapatikana kwa kiwango cha kuridhisha kutokana na Bajeti kubwa inayotengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa, ikiwa ni pamoja na asilimia 67% itokanayo na makusanyo ya fedha za vituo vya huduma ambayo hutumika kwa ajili ya ununuzi wa dawa.

HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO

Huduma hizi zimeendelea kutolewa katika vituo 54 kati ya vituo 61 kila siku ya kazi.

Utoaji wa huduma za chanjo na upimaji wa afya za watoto na akina mama wajawazito zimeendelea kutolewa kwa wananchi wanaoishi mbali na vituo  katika maeneo 22 huduma ambazo hujulikana kama  huduma za nje au (Mobile clinics) na huduma za mkoba 60 (Outreach Services).  Kiwango cha uchanjaji kwa  watoto wachanga na mama wajawazito kinaendelea vizuri kwa asilimia 94%.  Idadi ya akina mama wanaojifungulia vituoni inaendelea kuongezeka hadi sasa asilimia 89%. wamejifungulia vituoni.  Wahudumu wa afya wa vijiji ngazi ya  jamii  wanaendelea  kutoa  huduma ya kuelimisha  jamii juu ya kuwahi  katika vituo  vya kutolea  huduma za afya kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa rufaa pale wanapobaini kuwepo matatizo makubwa ya kiafya. Lengo la kufanya hivyo ni kutokomeza  vifo  vya akina mama wajawazito, watoto wachanga na watoto wenye umri chini ya miaka  mitano.

MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA MALARIA 

Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria yanaendelea. Ugunduzi wa ugonjwa wa malaria kwa kutumia vitendanishi ambavyo vinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya umefanyika. Dawa za tiba ya malaria zinapatikana katika vituo vya huduma kwa kiwango cha kuridhisha kwa zaidi ya 80%. Vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu vimegawiwa kwa wananchi kupitia shuleni. Wananchi wanaelimishwa umuhimu wa kupima kabla ya kutumia dawa kwani kipimo cha haraka cha kupima malaria kinapatikana katika vituo vyote. Wilaya ili endesha zoezi la unyunyiziaji wa dawa ya ukoko majumbani ili kuua mbu wa pevu waenezao ugonjwa wa malaria. 

MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI.

Mapambano dhidi ya maambukizi ya UKIMWI, vitendanishi vinaendelea kupatikana na kiwango cha maambukizi ni 0.7%.Wilaya imefanikiwa kupunguza kasi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kutokana na njitihada mbalimbali kama Upimaji wa hiari katika vituo vyote vya huduma za afya, Elimu ya kuzuia maambukizi katika mikutano mbalimbali ya jamii, Matumizi ya kinga kwa ajili ya kuzuia maambukizi kama vile mipira ya kiume na kike katika maeneo mbalimbali, Kuzuia maambukizi toka kwa mama mjamzito kwenda kwa mototo kwa kuwahimiza akina mama kwenda na wenza wao waendapo kliniki ya ujauzito.Wilaya imefanikiwa kuanzisha vituo 9 kwa ajili ya tiba ya kufubaza Virusi vya UKIMWI. Na dawa zinapatikana katika vituo hivyo mapambano hayo pia yamefanikiwa kutokana na ushirikiano mkubwa uliopo baina ya Halmashauri na Wadau waliopo Wilayani hasa Shirika la “Management Development for Health

 (MDH)”.

UPATIKANAJI WA RASILIMALI WATU

Idara ya afya inajumla ya watumishi 312 waliogawanyika katika kada mbalimbali kama ifuatavyo:-Daktari  6,madaktari  wasaidizi 11,Afisa wauguzi 2,Afisa wauguzi wasaidizi 43,wauguzi 107,tabibu 27 tabibu wasaidizi 5,katibu wa afya 2,afisa afya mazingira 1,afisa afya mazingira msaidizi 6,wafamasia 2,wateknolojia dawa 4,wateknolojia maabara  4,wateknolojia wasaidizi maabara 12,wateknolojia wasaidizi dawa 1 na watumishi wengine 73 ambao ni wahudumu wa afya n wasaidizi wa afya mazingira. Kulingana na ikama watumishi waliopo ni asilimia 40.8%.na upungufu wa watumishi ni kwa asilimia 59.2%.

MAFANIKIO

Kuwepo Kwa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara katika vituo vyote vya huduma.

Kiwango cha chanjo kimeongezeka hadi asilimia 94%

Upimaji wa VVU umeendelea kufanyika katika vituo vya huduma na kiwango cha maambukizi asilimia 0.7%

Idadi ya akina mama wanaojifungulia vituoni ni asilimia 89%.

Vipimo kwa ajili ya ugunduzi wa vimelea vya Ugonjwa wa malaria vinapatikana katika vituo vya huduma.

Ukarabati wa vituo vya Afya viwili Mabawe pamoja na Murusagamba.

Idara imepokea watumishi 33wapya wa kada mbalimbali za afya

CHANGAMOTO

Bado kuna upungufu wa watumishi katika vituo vya huduma kwa asilimia 59.2%. Tatizo hili limeongezeka kutokana na watumishi kuhama kwa kasi.

Ucheleweshaji wa fedha toka vyanzo mbali mbali

Ongezeko la vifo vya wazazi kulinganisha na miaka ya nyuma mwaka 2017  vilikuwa 7, mwaka huu Januari hadi Juni vimefika vifo 12, sababu kuu zikiwa ni uambukizo, kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua. Akina mama kutowahi kwenye vituo vya huduma kwa ajili ya kujifungua.

Ongezeko la wagonjwa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kisukari na magonjwa ya moyo.

 

MIKAKATI

Kuendelea kuomba vibali vya ajira toka Serikali

Kutoruhusu watumishi wengi kuhama kwa kuzingatia kwamba Wilaya ya Ngara iko pembezoni mwa Nchi, na inahitaji kupewa kipaumbele katika ajira.

Kuendelea kuelimisha wananchi, ili akinamama wajawazito waweze kuwahi vituo vya huduma  ili kusaidiwa na kupunguza vifo vya wazazi.

Kuelimisha wajawazito kuwahi kuanza kliniki mapema ili kugundua matatizo kama upungufu mkubwa wa damu, kifafa cha mimba na kuzuia matatizo hayo.

Kuelimisha/kuhamasisha jamii ili kujiunga na CHF iliyoboreshwa na hivyo kuongeza kipato katika vituo vya huduma.

UTEKELEZAJI WA HUDUMA ZA KIFUA KIKUU-AGOSTI 2018.pdf

IDARA YA AFYA - MTUHA JULAI 2017 - JUNI 2018.pdf

Idara ya Afya CHANJO.pdf

AFYA KINGA Julai 2017 - 2018.pdf

KITENGO CHA FAMASI IDARA YA AFYA.pdf

MENO NA KINYWA NGARA DC.pdf

Idara ta Afya Huduma ya Afya ya UZAZI NA MTOTO.pdf

LISHE NGARA DC.pdf

KITENGO CHA KUMBUKUMBU.pdf

USAFI MAZINGIRA.PROFILE(W) 2018.pdf



Matangazo

  • TANGAZO LA TATHMINI YA UJUZI NA UZOEFU KATIKA WILAYA YA NGARA KUTOKA TEMBO NICKEL August 30, 2022
  • MREJESHO WA MPANGO NA BAJETI YA HALMASHAURI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023 KWA KAMATI YA FEDHA, UTAWALA NA MIPANGO TAREHE 12 AGOSTI, 2022 September 23, 2022
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2022 HALMASHAURI YA WILAYA YA NGARA December 04, 2022
  • RIPOTI YA ATHARI ZA KIMAZINGIRA NA KIJAMII MRADI WA MAEGESHO YA MAGARI BENAKO December 01, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • WILAYA YA NGARA YANUNUA MAGARI KUTOKANA NA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI

    March 17, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU BAJETI YA HALMASHAURI 2023/2024 NGARA KAGERA

    March 07, 2023
  • KAMATI YA USHAURI YA WILAYA (DCC) YAPITISHA RASIMU YA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024

    February 22, 2023
  • MHE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT SAMIA SULUHU HASSAN ATOA PIKIPIKI KWA WATENDAJI WA KATA WILAYANI NGARA KAGERA.

    February 28, 2023
  • Tazama zote

Video

Moto Rusumo Agosti 2018
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa