- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Mkoani Kagera Mhe. Wilberd Bambara ameliongoza Baraza la Madiwani katika kikao cha robo ya pili Februari 3, 2026 katika ukumbi wa Halmashauri Mjini Ngara.
Katika kikao hicho Mwenyekiti pamoja na Baraza lake wamempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Solomon Kimilike kwa namna anavyosimamia Menejimenti ya Halmashauri hiyo katika usimamizi mzuri wa Miradi ya maendeleo.
Sambamba na hayo Madiwani hao wamepongeza mabadiriko makubwa yanayoendelea kuonekana kwenye halmashauri yao na kuongeza kuwa hali hiyo inasababishwa na usimamizi madhubuti wa watumishi.
Aidha wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanznaia Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika wilaya yao.

Mkiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe Wilbard Bambara katikati akiwa na Mkurugenzi mtendaji wilaya Ndg Solomon kimilike aliyesimama pamoja na Makamu mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Bi Theophilda

Waheshimiwa madiwani katika kikao cha Baraza robo ya pili 2025/2026

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe Wilbard Jobn Bambara

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Ndg Solomon O. Kimilike


www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa