- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Mhe. Wilbard Bambara, ameongoza kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili kilichofanyika Februari 3, 2026 katika ukumbi wa Halmashauri mjini Ngara.
Katika kikao hicho, Madiwani wamempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri, Ndg. Solomon Kimilike, kwa uongozi thabiti na usimamizi makini wa menejimenti unaochochea utekelezaji bora wa miradi ya maendeleo wilayani humo.
Wakichangia hoja mbalimbali, madiwani hao wameeleza kuridhishwa na mabadiliko makubwa yanayoonekana Ngara, wakibainisha kuwa mafanikio hayo yanatokana na uwajibikaji wa watumishi pamoja na usimamizi madhubuti wa rasilimali za umma.
Baraza hilo pia limeishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha nyingi zinazosaidia kusukuma mbele miradi ya maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi.
Katika kuimarisha uwajibikaji, madiwani waliuliza maswali ya papo kwa papo yakigusa sekta muhimu zikiwemo elimu, afya, maji na miundombinu hatua inayodhihirisha dhamira ya viongozi hao kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na maendeleo endelevu.



www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa