• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

Bi. Kapaya Awashukuru Wafanyakazi wa Nyamiaga na Murgwanza

Wakati ilipowekwa: April 6th, 2018

Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi hapa nchini Ndugu Chansa Kapaya, amewashukuru wafanayakazi wa hospitali za Nyamiaga na Murgwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, kwa huduma na ushirikiano walioonesha kwa majeruhi wa ajali ya basi.

Bi. Kapaya ameyasema hayo Aprili 03, 2018, wakati wa mazishi ya wakimbizi sita walioaga dunia kwa ajali ya basi, iliyotokea Machi 29, 2018 katika kijiji cha Kasharazi, wakitokea katika kambi ya wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo mkoani Kigoma na kuzikwa Benaco Ngara.

Alisema shirika la kuhudumia wakimbizi, kwa kushirikiana na mashirika mengine, wamejitahidi kuokoa maisha ya majeruhi, ikiwa ni pamoja na kukodi ndege ya kuwasafirisha waliopewa rufaa kwenda hospitali ya Bugando.

“Tunawashukuru wahudumu wa hospitali za Nyamiaga na Murgwanza, pamoja na serikali ya wilaya, na kwa namna ya pekee wanakijiji cha Rwakalemela, waliotoa eneo la kuwahifadhi wenzetu; Mwenyezi Mungu awabariki.” Alisema Bi. Kapaya.

Aidha, Mkurugenzi wa Idara ya Kuwahudumia Wakimbizi Wizara ya Mambo ya Ndani hapa Nchini Ndugu Harison Mseka, alisema kwamba jumla ya wakimbizi 21,000, wamerejea nchini Burundi kutoka kwenye kambi za wakimbizi mkoani Kigoma tangu Septemba 2017.

Alisema kila wiki wakimbizi 2,000 wanatakiwa kurejea nchini Burundi, sawa na 8,000 kwa mwezi, na kuongeza kwamba mwaka jana walilenga kurejesha wakimbizi 12,000, lakini walifanikiwa kuwarejesha wakimbizi 13,300.

Ndugu Mseka alisema mwaka huu wanalenga kuwarejesha wakimbizi wapatao 80,000, ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano waliojiwekea kwa mwaka huu.

Amefafanua kwamba majeruhi 26 wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Murugwanza, na Hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza, ambapo wengine wako katika kambi ya Lumasi.

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • DC NGARA MHE COL MATHIAS KAHABI AKUTANA NA BRIG GEN GABRIEL E. KWILIGWA - KAMANDA BRIGDE YA MAGHARIBI.

    May 16, 2025
  • MHE COL MATHIAS JULIUS KAHABI DC NGARA ASHIRIKI USAFI NA WANANCHI WA NAKATUNGA

    May 15, 2025
  • MWENYEKITI WA CCM AENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO - NGARA

    May 16, 2025
  • KIKAO KAZI CHA UTEKELEZAJI WA MRADI WA AFUA ZA LISHE WA KILIMO CHA MAHINDI CHAFANYIKA - NGARA

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa