- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
17/01/2026
Leo Siku ya Jumamosi lifanyika Bonanza la Michezo mbalimbali katika kiwanja cha Halmashauri na uwanja Posta Ngara Mjini.
Ambapo ilianza Jogging iliyoshirikisha watumishi mbalimbali wakulima, wafugaji na wajasilimali .Jogging ilihitimishwa kwa kufanya mazoezi ya pamoja ( Aerobic)
Bananza hilo la michezo liliendelea kwa Mbio fupi na Kuvuta Kamba kati ya watumishi wa Halmashauri VS Ngara Security ambapo Watumishi Halmashauri walishinda 2 dhidi ya Ngara Security.
Bananza lilihitimishwa kwa mchezo wa soka kati ya Timu ya watumishi Makao makuu Vs watumishi Walimu ambapo matokeo TIMU YA WATUMISHI MAKAO MAKUU Walishinda Magoli mawili 2 Dhidi ya TIMU YA WALIMU SC 0 , wafungaji katika mchezo huo ni Eng Gerlad Ndyetabula kutoka _ Miundo mbinu Maendeleo Mjini na Vijijini goli la 1 na goli la 2 lilifungwa na Chacha Paulo kutoka ofisi ya Ardhi.
Mchezaji bora alikuwa ni Nahodha wa Timu ya Watumishi Makao Makuu Ndg Ally Mbape kutoka Idara ya Utawala.




www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa