- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kwa mara ya kwanza katika katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa shule za msingi, mchezo wa Cricket umejumuishwa katika michezo inayoshindaniwa.
Mchezo huo ambao unafanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Lugalo, inajumuisha timu 4 kutoka Mikoa ya Morogoro, Tanga,Dar es Salaam na Dodoma.
Katika michezo iliyochezwa leo Juni 10, 2025 Timu ya Cricket ya Mkoa wa Dodoma Wavulana ilishinda mikimboa 119 kwa 48 dhidi ya Dar es Salaam.
Mchezo mwingine wa Wavulana ulizikutanisha timu za mikoa ya Tanga na Morogoro, na Tanga iliibuka na ushindi wa Mikimbio 98-90.
Kwa upande wa Wasichana, timu ya Cricket ya Mkoa wa Morogoro ilikutana na Tanga, ambapo Morogoro iliibuka na ushindi wa 37 kwa 36, katika mchezo wa mwisho kwa siku ya leo.
Mratibu wa Cricket kwenye UMITASHUMTA 2025, Hamis Hassan Abdallah ameelezea faida ya mchezo huo, ikiwa ni pamoja na kuandaa wachezaji wa timu ya Taifa kwa miaka ijayo.
"Huu ni mchezo mpya, na mwaka huu utakuwa kwenye UMITASHUMTA pekee, ila mwakani tutajumuisha pia kwenye UMISSETA, lengo ni kuzidi kuutangaza na kuwavutia wanafunzi wengi zaidi kucheza" amesema Hassan
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa