• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

DAFTARI LA WAPIGA KURA KUANZA KUBORESHWA JULAI MWAKA HUU.

Wakati ilipowekwa: May 15th, 2024

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza na waandishi wa habari Mjini Unguja, Zanzibar, leo tarehe 15 Mei, 2024, ambapo ametangaza kuwa uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika tarehe 01 Julai, 2024.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele (katikati) akizungumza na waandishi wa habari Mjini Unguja, Zanzibar, leo tarehe 15 Mei, 2024, ambapo ametangaza kuwa uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika tarehe 01 Julai, 2024. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Bw. Kailima R. K na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji (Rufaa) Mstaafu, Mbarouk Salim Mbarouk.



Wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika mkutano huo na Waandishi wa Habari.


Uzinduzi wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika tarehe 01 Julai, 2024 mkoani Kigoma na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB).

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Unguja, Zanzibar, leo tarehe 15 Mei, 2024, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele amesema kuwa zoezi hilo litakapokamilika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linatarajiwa kuwa na wapiga kura 34,746,638.

“Kwa kuzingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Daftari linatarajiwa kuwa na wapiga kura 34,746,638 kutoka 29,754,699 ya mwaka 2020 hili ni ongezeko la wapiga kura wapya 5,586,433 sawa na asilimia 18.7,” amesema Jaji Mwambegele.

Ameongeza kuwa katika zoezi hilo wapiga kura 4,369,531 wanatarajiwa kuboresha taarifa zao na wapiga kura 594,494 wataondolewa katika Daftari kwa kupoteza sifa za kuwa wapiga kura.

Kuhusu idadi ya vituo, Jaji Mwambegele ameseama Tume ilifanya uhakiki wa vituo vya kuandikishia wapiga kura mwaka 2023 ambapo baada ya zoezi hilo iliamuliwa kuwa vituo vya kupigia kura vitakavyotumika kwenye uboreshaji wa Daftari ni 40,126.

“Kabla ya uhakiki huo wa vituo, kulikuwa na vituo 37,814 ambavyo vilitumika kuandikisha wapiga kura mwaka 2019/2020. Baada ya zoezi hilo la uhakiki, jumla ya vituo 40,126 vitatumika kwenye zoezi la uboreshaji wa Daftari mwaka 2024/2025 ambapo kati ya vituo hivyo, 39,709 ni vya Tanzania Bara na vituo 417 ni vya Zanzibar,” amesema Jaji Mwambegele.

Amefafanua kuwa siku ya uzinduzi ndiyo siku ambayo pia uboreshaji utaanza katika mkoa wa Kigoma na kuendelea katika mikoa mingine ya Katavi, Rukwa na Tabora.

“Kwa lengo la kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi, uboreshaji utafanyika kwenye mizunguko 13 itakayobainishwa kwenye ratiba. Aidha, zoezi hili litaendeshwa kwa siku saba kwenye kila kituo cha kuandikisha wapiga kura,” amesema Jaji Mwambegele.

Amesema kuwa zoezi hilo litahusu kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 pamoja na wale ambao hawajapoteza sifa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi au sheria nyingine yeyote.

“Zoezi hilo pia litatoa fursa kwa wapiga kura waliandikishwa awali na ambao wamehama kutoka mkoa au wilaya moja kwenda nyingine waweze kuhamisha taarifa zao kutoka kata au jimbo walioandikishwa awali na kutoa fursa kwa wapiga kura walioandikishwa kurebisha taarifa zao yakiwemo majina….,” amesema Jaji Mwambegele.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa zoezi hilo la uboreshaji wa Daftari litahusisha pia kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza au kadi zao kuharibika na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuukana uraia wa Tanzania na kifo.

“Kwa upande wa Zanzibar uboreshaji wa Daftari utamhusu mtu yeyote aliyepo Zanzibar ambaye hana sifa za kuandikishwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar lakini ana sifa ya kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano,” amesema Jaji Mwambegele.

Amesema Tume imefanya ununuzi wa vifaa vya uandikishaji ikiwemo ununuzi wa BVR Kits 6,000 zinazotumia vishikwambi kuchukua taarifa za wapiga kura ikiwemo picha, saini na alama za vidole.

“Tofauti na mashine za BVR zilizotumika katika uboreshaji wa mwaka 2015 na 2020 zilizokuwa na uzito wa kilo 35, BVR Kits za awamu hii ni nyepesi zenye uzito wa kilo 18 ambazo zitaweza kubebeka kwa urahisi,” amesema Jaji Mwambegele.

Amesema, Tume imeanzisha mfumo wa uboreshaji kwa njia ya mtandao uitwao Online Voters Registration System (OVRS) ambao utamuwezesha mpiga kura aliyemo kwenye Daftari kuanzisha mchakato wa awali wa kuboresha taarifa zake kwa njia ya mtandao kwa kutumia simu ya mkononi au kompyuta.

“Baada ya kukamilisha mchakato kwa njia ya mtandao mpiga kura atalazimika kufika kituo cha kuandikisha wapiga kura ili kukamilisha mchakato na kupatiwa kadi yake ya mpiga kura,” amesema Jaji Mwambegele.

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • DC NGARA MHE COL MATHIAS KAHABI AKUTANA NA BRIG GEN GABRIEL E. KWILIGWA - KAMANDA BRIGDE YA MAGHARIBI.

    May 16, 2025
  • MHE COL MATHIAS JULIUS KAHABI DC NGARA ASHIRIKI USAFI NA WANANCHI WA NAKATUNGA

    May 15, 2025
  • MWENYEKITI WA CCM AENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO - NGARA

    May 16, 2025
  • KIKAO KAZI CHA UTEKELEZAJI WA MRADI WA AFUA ZA LISHE WA KILIMO CHA MAHINDI CHAFANYIKA - NGARA

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa