- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo Mkuu wa Wilaya ya Ngara Col, Mathias J. Kahabi akiwa na katibu Tawala wilaya Bi. Hatujuani A Lukali, Afisa Elimu Sekondari Mwl.Enock Ntakisigaye aliyewakilisha Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Ndg Solomon Kimilike, Dso, Ocd, Pccb, Afisa elimu Msingi Bi Josline Bandiko, Maafisa elimu Taaluma Msingi na Sekondari.
Mhe Dc Kahabi amefanya kikao kazi na Wakuu wa shule zote za sekondari , walimu wakuu wa shule zote za Msingi wilayani, Maafisa elimu kata zote na watendaji wa kata zote.
Kikao hicho kimefanyika ukumbi wa shule ya Sekondari Ngara Uliopo Ngara mjini.
Lengo la kikao kazi hicho ilikuwa ni kuweka Mkakati wa kuinua taaluma shule za Msingi na sekondari pia kupitia matokeo ya kumaliza Elimu Msingi na upimaji Darasa la 4, matokeo ya kidato Cha 6,4 na matokeo ya upimaji kidato Cha pili.
Aidha yamefanyika Majadiliano Mbalimbali baada ya Majadiliano imewekwa mikakati ya kuboresha Elimu wilayani ambayo ni:
1. kutoa motisha Kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri.
2. Kuwa na mitihani ya pamoja ya Wilaya Kwa shule za Msingi na sekondari.
3. Wanafunzi wote kupatiwa chakula Cha mchana Kwa kushirikisha wazazi na wadau wengine.
4. Shule kutoa mazoezi Kila siku Kwa wanafunzi.
5. kamati za kudhibiti utodo za wilaya na kata kuanza kufanya kazi mara moja kuthibiti utoro.
6. Kuwepo Kwa msawazo wa Walimu ili kupunguzwa tatizo Kwa shule zenye walimu wachache.
7. uwa na mitihani ya pamoja ya Wilaya Kwa shule za Msingi na sekondari.
Mwisho Mkuu wa Wilaya Mhe Col.Kahabi aliwataka kufanyiwa kazi mikakati yote pia alisisitiza usimamizi madhubuti wa miradi ya Maendeleo inayopekekwa shuleni moja Kwa moja.
Aidha Mhe Col. Kahabi alimshukuru na Kumpongeza Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassani Kwa jitihada zake kuleta Miradi ya maendeleoi Wilayani Ngara ikiwa Ujenzi wa vyumba vya Madarasa Shule za zamani na Ujenzi wa Shule Mpya, matundu ya vyoo, nyumba za walimu na utengdnezaji wa Madawati, wilayani.
Walimu wakuu wa shule za Msingi , Wakuu wa shule za sekondari, maafisa elimu kata, na watendaji wa kata wakiwa kwenye kikao kazi kilichoongizwa na Mhe Col Mathias J Kahabi ukumbi wa Ngara sekondari.
Wakuu wa shule ,walimu Wakuu wakiwa kwenye Kikao kazi kilichofanyika Ngara sekondari.
Mkuu wa wilaya Mhe Col. Mathias J Kahabi aliyesimama akiongea na walimu Wakuu, Wakuu wa shule, Maafisaelimu Kata, watendaji Kata katika Kikao kazi kilichofanyika Ngara sekondari.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa