- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 18/9/2025,
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara amepokea ugeni wa Makamanda wa Jeshi toka Rwanda na Tanzania ambao wapo kwa Kikao cha kawaida cha ujirani mwema kinachofanyika Wilayani Ngara.
Kikao hicho cha siku mbili kilianza tarehe 17/9/2025 na kimeongozwa na Kamanda wa Brigade ya Magharibi Brig Gen Gabriel Kwiligwa pamoja na Wakuu wa Vikosi vya JWTZ Biharamulo na Kaboya.
Aidha, kwa upande wa Rwanda Kamanda wa Division ya Mashariki ya Jeshi la RDF alihudhuria Kikao hicho pamoja na Makamanda wa ngazi ya juu walioko kwenye eneo lake la uwajibikaji.
Makamanda wote toka Tanzania na Rwanda kwa pamoja wamepongeza shughuli za ulinzi na usalama katika mipaka yote ya nchi mbili zinazofanywa na Makamanda na askari na kuahidi kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano wa hali ya juu ili kuondoa kabisa changamoto ndogo ndogo pindi zinapojitokeza.
Ngara kazi inaendelea..
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa