- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Ndg Charles Kichere Tarehe 09/7/2025, alifanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo uliopo katika maporomoko ya mto Kagera Wilayani Ngara.
Aidha, Controller and Auditor General (CAG) huyo alifuatana na CAG wenzake toka nchi za Rwanda na Burundi ambao ni wadau wakubwa katika mradi huo uliojengwa na kunufaisha wananchi wa nchi zote tatu.
CAG wote toka Tanzania, Rwanda na Burundi walifanya Kikao cha pamoja katika Makao Makuu ya RPCL yalipo Rusumo - Tanzania na baadae walipokea taarifa mbalimbali toka kwa watalaam wa RPCL na mwisho walitembelea mradi wa ukarabati/ujenzi wa nyumba za wananchi zilizoathiriwa na ulipuaji wa miamba wakati wa ujenzi wa mradi.
Ziara hiyo kwa waathirika wa mradi ilifanyika kwa pande zote mbili za Tanzania na Rwanda na kupongeza hatua nzuri iliyofikiwa katika ujenzi huo.
Ngara kazi inaendelea
www ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa