- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
9/7/2025
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara amefungua mafunzo ya awali ya Jeshi la akiba(Mgambo) katika kijiji cha Kasharazi, Kata ya Rusumo, Tarafa ya Nyamiaga.
Akitoa taarifa ya ufunguzi wa mafunzo hayo Capt Luambano Mshauri wa JA, Wilaya ya Ngara amesema idadi ya wanafunzi waliopo ni 67 kati yao wanaume 59 na wanawake 8 na kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika mafunzo hayo yalichelewa kufunguliwa.
Aidha, Mhe Col Mathias Julius Kahabi amewapongeza Viongozi wa Serikali ya kijiji, wakufunzi, wanafunzi pamoja na wananchi kwa ujumla kwa kukubali mafunzo hayo kufanyika kijijini hapo na kuwaomba kuendelea kuwapa kila aina ya support wanafunzi na wakufunzi hao ili wamalize vema na kuwa tayari kwenda kutumikia wananchi kwa uzalendo wa hali ya juu.
www ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa