- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
LEO TAREHE 28/7/2025,
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara akifuatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, wawakilishi wa RPCL, Viongozi wa Serikali ya Kijiji/Kata Rusumo pamoja na Wakandarasi Kampuni ya AZHAR na Kampuni ya KIKA wanaotekeleza ujenzi/ukarabati wa majengo(structures) idadi 592 yaliyoathiriwa na ulipuaji wa miamba wakati wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo, sasa ujenzi/ukarabati wa majengo hayo ya wananchi wa Rusumo umekaribia kukamilika.
Hadi sasa zaidi ya nyumba idadi 490 zimeshakamilika na kukabidhiwa kwa waguswa wa mradi huo ambapo nyumba zilizobakia idadi 102 ziko hatua za mwisho za ukamilishaji na muda mchache ujao zitakuwa tayari na kukabidhiwa kwa wananchi.
Aidha, Mhe Col Mathias Kahabi DC Ngara amewaagiza Wakandarasi Kampuni ya AZHAR na Kampuni ya KIKA kukamilisha ujenzi/ukarabati huo haraka iwezekanavyo. Pia amawataka wananchi wenye changamoto na ukarabati wa nyumba zao watoe taarifa mapema ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kabla Wakandarasi hawajakabidhi mradi na kuondoka.
Ngara kazi inaendelea.
www ngaeadc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa