- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
HABARI LEO
08/04/2025
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara ametembelea Kituo kipya cha ukaguzi cha Uhamiaji - Sekeseke na kuongea na Maafisa na askari wa Polisi na Uhamiaji waliopo katika Kituo hicho.
Kituo kipya cha ukaguzi cha Uhamiaji Sekeseke kimeanzishwa hivi karibuni kwa lengo la kuongeza ufanisi katika shughuli za Ulinzi na Usalama wa Mpaka wetu na nchi jirani.
Aidha, Mhe DC Kahabi amewapongeza maafisa na askari wa Polisi na Uhamiaji walioko katika Kituo hicho kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa uzalendo na Weledi wa hali ya juu na kuwataka wasivunje maadili na taratibu za kazi yao.
Pia ameagiza(Uhamiaji) wasiruhusu wahamiaji haramu toka nchi jirani kuingia nchini mwetu bila kufuata taratibu na sheria za Uhamiaji za nchi yetu.
Mhe Col Mathias Kahabi Dc Ngara akiwa na Afisa uhamiaji Wilaya Salehe walipotembelea sekeseke
Mhe Col kahabi akiwa na Maafisa wa Jeshi la uhamiaji walipotembelea Sekeseke
Ngara Kazi inaendelea..
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa