- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 10/3/2025, Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara amekutana na baadhi ya wafugaji pamoja na Viongozi wao kwa lengo la kutatua KERO ya wizi wa mifugo unayoendelea katika vijiji vya Rwakaremela na Kasulo, Kata ya Kasulo.
Viongozi wa wafugaji pamoja na baadhi ya wafugaji walikutana ofisni kwa DC pamoja na wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya ambapo walipata fursa ya kueleza changamoto kubwa ya wizi wa ng'ombe ambao umekuwa ukifanywa na wafugaji wenzao.
Viongozi wa Serikali ya kijiji na Kata wamesema tatizo hili lipo na kwamba wanakamilisha vikao vya kisheria ili waweze kuazimia hatua za kuchukua dhidi ya wafugaji wachache wanaohusika na wizi huo.
Mhe Col Mathias Kahabi DC Ngara, amekubaliana na hatua hiyo ya Viongozi wa Serikali za vijiji vya Rwakaremela na kwamba watakapowasilisha hayo maazimio atayafanyia kazi kupitia Kamati ya Usalama ya Wilaya.
Aidha, ameonya tabia ya wafugaji wachache wanaojihusisha na wizi wa ng'ombe toka kwa wafugaji wenzao waache mara moja kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mhe Col Mathias kahabi DC Ngara katika picha ya pamoja na kamati ya usalama wilaya,viongozi wa kata kasulo na wafugaji
Ngara Kazi inaendelea..
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa