- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
01/08/2025
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Ndg. Solomon O. Kimilike leo ametembelea Hospitali ya Nyamiaga iliyopo Ngara Mjini ambapo alifuatana na Afisa afya Mkoa wa kagera Ndg Yasin Mwinory , Afisa Chanjo Mkoa Ndg Salum kimbau, Mhandisi wa Ujenzi Eng Sanga na Dr Tira.
Lengo la ziara hiyo ikiwa ni kukagua miradi ya (SRWSS) Sustanable Rural water supply and Sanitation 2024/2024. Aidha Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Kimilike na viongozi wa Mkoa aliyofuatana nao walitembelea na kukagua miradi ifuatayo
1. Sehemu ya kunawia Mikono ili kudhibiti magonjwa ya Mlipuko.
2.Ujenzi wa watundu ya vyoo vikiwemo vya walemavu
3. Mfumo wa uhakika wa upatikanaji maji safi na salama katika Hospital
4. Ukarabati wa Jengo la kujifungulia (Labour ward)
5.Ukarabati wa Jengo la Upasuaji( Theatre)
6. Ukarabati wa Jengo la akina mama wanaosubiri kujifungua.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya Ndg Kimilike alimpongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe Dr Samia Suluhu Hassan kwa fedha za ukarabati katika Wilaya wa Ngara.
Aliyeko mbele Afisa Afya Mkoa Ndg Yasin Mwinory akifuatiwa na Afisa Chanjo Mkoa Ndg Salum Kimbau , Mkurugenzi Mtendaji H/Wilaya Ndg Solomon O. Kimilike, Dr Tira wa Nyamiaga Hospital na Eng Sanga kutoka Halmashauri wakitembelea kukagua
Wakiangalia ukarabati uliofanyika katika Hospitali ya Nyamiaga
Wakitembelea Jengo la kujifungulia katika Hospitali ya Nyamiaga
Jengo la Upasuaji Nyamiaga Hospitali
Vyoo
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa