• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

DKT. MWIGULU: TANZANIA NI MALI YETU SOTE, SI MALI YA SERIKALI WALA CHAMA CHA SIASA

Wakati ilipowekwa: November 26th, 2025

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania ni mali ya Watanzania wote wala si ya Serikali au chama cha siasa na hivyo kila mmoja anapaswa kuilinda.

“Tanzania si mali ya Serikali, Tanzania si mali ya chama cha siasa na vyama vya siasa vipo kwa sababu nchi ipo. Tuilinde nchi yetu. Mungu ametupa nchi nzuri na kila mmoja ana wajibu wa kuilinda,” amesisitiza.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo jioni (Jumanne, Novemba 25, 2025) wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali nchini katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Amesema fedha zinazotumika kujenga miundombinu ya barabara, zahanati, vituo vya afya, miradi ya maji ni za Watanzania na wala si za Serikali. “Hakuna fedha ya Serikali kwenye miradi. Fedha yote inayotekeleza miradi ni yako Mtanzania isipokuwa inasimamiwa na Serikali.”

Amesema kila Mtanzania anachangia pato la Taifa na anajinyima aina fulani ya maisha ili kujenga barabara au zahanati kwenye eneo lake. “Ukinunua shati kuna sehemu unapeleka kujenga barabara, unakuwa umetenga sehemu ya kutumia na sehemu umejinyima ili kuchangia maendeleo ya nchi.”

Akielezea madhara ya vurugu zilizotokea Oktoba 29, mwaka huu, Waziri Mkuu amesema vitendo vile vililenga kuhujumu uchumi wa nchi na vimesababisha uharibifu mkubwa wa mali ikiwemo kuchoma ofisi za serikali 756; vituo vya mabasi ya mwendokasi 27; mabasi sita; nyumba za watu binafsi 273; vituo vya polisi 159; vituo vya mafuta 672; magari ya watu binafsi 1,642; pikipiki 2,268; magari ya serikali 976 zikiwemo ambulance.

Amesema maisha ya Mtanzania mmojammoja yanahusisha mtu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili kujipatia riziki zao. “Maisha ya Mtanzania ni ya kutoka eneo moja aende eneo jingine; haya si maisha ya Serikali, ni maisha ya Mtanzania mmoja mmoja. Maisha ya mwana Dar es Salaam ni kutoka hatua moja kwenda nyingine. Hakuna Mtanzania ambaye amejilimbikizia mali kwamba anaweza akakaa mwaka mzima bila kutoka. Atatoka Mbezi aende Posta, atatoka Kimara aende Kariakoo, atatoka Kariakoo aende Goba. Hawa watu wasipotoka unataka wale nini?”

Amesema uharibifu wa miundombinu uliofanyika ulilenga kuua uchumi wa nchi. “Kwamba mpango uliwekwa pasiwe na miundombinu ya hawa watu kusafiri. Je, watakula nini? Walipanga kuchoma stendi ya mabasi ya Magufuli, kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi na reli ya SGR. Hizi siyo mali za Serikali, ni mali za umma. Hivi unapochoma kituo cha DAWASCO kinachowapa maji safi na salama unataka hawa watu waishije?” alihoji Waziri Mkuu.

Dkt. Mwigulu amewasisitiza Watanzania wawe mstari wa mbele kuilinda Tanzania kwa kutoa taarifa pale wanapobaini watu wasiofahamika kwani hivi sasa hawafikii kwenye nyumba za kulala wageni.

“Niwaelekeze viongozi wa Serikali ngazi zote kuanzia wa mitaa, kitongoji na wa kijiji wawe macho; hawa watu wabaya wabaya hawafikii tena kwenye nyumba za wageni, wanafikia kwa mtu mmoja mmoja. Kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake, kwa kujua kuwa huyo aliyemleta ni nani.” 

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema wale wasioitakia mema Tanzania wanatamani mabaya zaidi yaendelee kutokea, hivyo ni busara kuwakataa kwa kuwa wana dhamira ya kufanya uovu dhidi ya Tanzania. “Natamani kila mmoja alibebe jambo hili kwa ukubwa, hawa watu hawatupendi, wanaangalia rasilimali zetu. Tukumbuke kuwa nchi yetu siyo masikini, kuna watu wanamezea mate rasilimali zetu. Ninawahakikishia kuwa tutailinda Tanzania na rasilimali zake kwa gharama yoyote ile, watameza mate hadi yataisha,” amesisitiza.

Amesema kuwa watumishi wa umma wanapaswa kubadilisha mtazamo kuhusu sekta, kuiheshimu na kuacha kuwaona walioko kwenye sekta hiyo ni watu wa chini. “Hatutaushinda umasikini kama tutaamini kwamba sekta binafsi ni maadui, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amebadilisha sheria inayomruhusu mkandarasi mzawa apate mradi mkubwa na wale wakubwa waombe sub-contract kwake, hili litatengeneza fursa za ajira kwa vijana wengi wa Kitanzania,” amesisitiza Dkt. Mwigulu.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri na Naibu Mawaziri kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja viongozi wa Jukwaa la Wahariri

www.ngaradc.go.tz

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • DKT. MWIGULU: TANZANIA NI MALI YETU SOTE, SI MALI YA SERIKALI WALA CHAMA CHA SIASA

    November 26, 2025
  • NDG. SOLOMON KIMILIKE DED-NGARA ASHIRIKI KUPIGA KURA UCHAGUZI MKUU 2025 NA KUHAMASISHA WANANCHI.

    October 29, 2025
  • DC NGARA AHAMASISHA VIJANA BODABODA KUJITOKEZA KESHO KUPIGA KURA

    October 28, 2025
  • SALAMU ZA SHUKRANI KWENDA MBEYA.

    October 16, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa