• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

GST YATOA ELIMU YA MAJANGA YA ASILI MANYARA

Wakati ilipowekwa: October 9th, 2023

GST yatoa wito kwa wananchi kupata elimu ya Majanga ya Asili

Katika kuadhimisha Wiki ya Maafa Duniani, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeanza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu athari za majanga ya Asili ya jiolojia hususan Matetemeko ya Ardhi ambayo hutokea katika maeneo mbalimbali nchini kwakuwa nchi yetu imepitiwa na Ukanda wa Bonde la Ufa la Afrika Mashariki.


Maonyesho hayo yameanza leo Oktoba 09, 2023 mjini Babati Mkoa wa Manyara na yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi Oktoba 10, 2023 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.


Akizungumza katika maonesho hayo, Meneja wa Sehemu ya Mapping & Economic Geology na Mkuu wa Kitengo cha Majanga ya Asili ya jiolojia kutoka GST Bw. Gabriel Mbogoni amesema GST imeshiriki maonyesho hayo ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Majanga ya Asili ya Jiolojia kwa lengo la kupunguza athari zitokanazo na majanga hayo hususan katika kipindi hiki ambacho kumetolewa tahadhari ya uwezekano wa kutokea kwa mvua za Elnino.


Katika hatua nyingine Mbogoni ametoa wito kwa wananchi kutembelea banda la GST ili kujifunza na kupata uelewa wa majanga ya Asili ya Jiolojia.


Maonesho hayo hufanyika Mwezi Oktoba Kila Mwaka ambapo kwa Mwaka huu yanafanyika Mjini Babati Mkoani Manyara ambapo yamebebwa na Kauli Mbiu isemayo *"Imarisha Usawa kwa Uthabiti Endelevu"* ambapo Kauli Mbiu hiyo inalenga kuhamasisha umuhimu wa kuwa na mikakati thabiti ya kupambana na umaskini na ukosefu wa usawa ili kuweza kupunguza athari za maafa zitokanazo na matokeo ya umaskini,

ukosefu wa usawa na ubaguzi.


Maonesho hayo yanakwenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Vijana yaliyobebwa na Kauli Mbiu isemayo *"Vijana na Ujuzi Rafiki wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu"* pamoja na kilele cha mbio za Mwenge.




Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • MHE. COL MATHIAS KAHABI DC NGARA AKUTANA NA BALOZI WA RWANDA.

    May 29, 2025
  • NGARA YAENDELEA VIZURI NA MICHEZO YA SHULE ZA MSINGI UMITASHUMTA NGAZI YA MKOA.

    May 26, 2025
  • MADEREVA WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI ILI KUPUNGUZA AJALI - NGARA

    May 24, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI - MTUMBA DODOMA

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa