• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

Hakuna Mwanafunzi Kubaki Nyuma Wote Wafaulu Kwa asilimia 95; REO Kagera

Wakati ilipowekwa: January 29th, 2019

Idara ya Elimu msingi na sekondari mkoani Kagera, imeazimia kufaulisha  kwa asilimi 95 kwa wanafunzi, watakaofanya mtihani wa Taifa wa darasa la nne na  saba, pia kufuta daraja  la nne na sifuri kwa wanafunzi, watakaohitimu kidato cha nne mkoani humo.

Azimio hilo limewekwa wazi Januari 28 ,2019 na Afisa Elimu wa Mkoa wa Kagera  Ndugu Aloyse Kamamba, alipokutana na walimu wa vitengo mbalimbali na maafisa elimu wa halmashauri ya wilaya ya Ngara, akiwa katika ziara ya kuhamasisha uboreshaji wa taaluma.

Ndugu Kamamba  amesema;  walimu wanatakiwa kufundisha kwa kutumia mbinu shirikishi na vifaa kwa kila somo, wakilenga kufaulisha wanafunzi, huku wakihakikisha hakuna wanafunzi wanaobaki nyuma kitaaluma, na kuwasaidia wazito kuelewa.

“Naomba niwe wazi kwa hili, mwalimu atakayeshindwa kutekeleza malengo tuliyojiwekea kimkoa, hana budi kutafuta kazi nyingine kabla ya hatujamuondoa, kwani atakuwa hakusanyi pamoja nasi, bali anatawanya” Alisema Kamamba

Amesema serikali imewekeza katika sekta ya elimu, ambapo indara ya elimu mkoa wa Kagera inapokea zaidi ya Shilingi bilioni 1.5; hivyo hakuna kiongozi, atakayemvumilia mwlimu mzembe, katika utekelezaji wa mikakati ya kufaulisha wanafunzi.

Katika hatua nyingine, amewapongeza walimu kwa juhudi wanazofanya katika utendaji kazi; licha ya chanhgamoto mbalimbali wanazokabiriana nazo kama vile kufanyakazi katika mazingira magumu.

“Kwa ujumla mkoa wetu umefanya vizuri kwa kushika nafasi ya nane kati ya mikoa 31, na mwaka juzi tulikuwa nafasi ya tisa, kwa hiyo, tumepanda nafasi moja, nafasi moja hii si haba, kwa sababu mikoa yote inajitahidi kufanya vizuri.” Alisema Ndugu Kamamba.

Kuna baadhi ya Halmashauri, ambazo hazikutimiza wajibu wao, kwa mfano, Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Muleba, Bukoba Vijiijini, na Kurwa, amesema uwajibikaji wa halmashauri hizo ulikuwa hafifu, huku akidai kwamba wamefanya vikao kazi na Halmashauri hizo kuona kwamba mwaka 2019 wanafanya vizuri zaidi.

Katika vikao kazi hivyo amesema kwamba kwa wasiotimiza wajibu wao hatua inayofuata ni kuwawajibisha kisheria na kwamba kila mmoja azibe pengo alilolitengeneza mwaka 2018, ili mkoa uweze kufanya vizuri mwaka 2019.

Kupanda na kushuka kwa Mkoa wa Kagera katika mitihani ya Taifa, kunatokana na uwajibikaji hafifu wa viongozi ngazi za wilaya, lakini maafisaelimu kata nao hawatimizi wajibu wao ipasavyo pamoja na kupewa vitendeakazi, pia walimu wakuu wasipotimiza wajibu wao, matokeo yanayopanda na kushuka.

“Kielimu tuko vizuri kimkoa, mwaka 2018; mtihani wa darasa la nne mkoa wetu, umeshika nafasi ya kwanza, lakini mithani wa dararsa la saba umeshika nafasi ya tano; kidato cha pili mkoa umeshika nafasi ya saba, laikini kidato cha nne umeshika nafasi ya nane.” Alisema Ndugu Kamamba.

Mwaka 2018 Mkoa huo ulipanga kuwa na ufaulu wa asilimia 88 ambapo  wanafunzi 25,499 wamejiunga na kidato cha kwanza 2019 katika  awamu ya kwanza kwa kuzingatia vyumba vya madarasa vilivyopo, kati yao  wavulana ni 14,356 na wasichana 13,143 sawa na asilimia 64.4 .

Vile vile Afisa Taaluma wa mkoa wa Kagera Ndugu Fidelis Apolinary, amewataka walimu kufuata taratibu na miogozo iliyowekwa na serikali, kuhakikisha watoto wanafaulu; badala ya kusingizia changamoto zilizomo katika sekta ya elimu.

“Visingizio vya kutopandishwa madaraja na mishahara, havina maana, kwani hapa Tanzania hakuna mkoa wowote walimu, walipopandishwa madaja wala kuongezewa mishahara, lakini mkoa wa Kagera, tumekuwa wa nane wakati kuna mkoa umekuwa wa kwanza, tuwajibike.” Alisema Apolinary.

Pia, katika kikao hicho walimu wa mkoa huo, kwa kushirikiana na wazazi, wameagizwa kuanzia Marchi 31 mwaka huu, wanafunzi wapate chakjula au uji shuleni, na utekelezaji wake usimamiwe na wananchi.

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • DC NGARA MHE COL MATHIAS KAHABI AKUTANA NA BRIG GEN GABRIEL E. KWILIGWA - KAMANDA BRIGDE YA MAGHARIBI.

    May 16, 2025
  • MHE COL MATHIAS JULIUS KAHABI DC NGARA ASHIRIKI USAFI NA WANANCHI WA NAKATUNGA

    May 15, 2025
  • MWENYEKITI WA CCM AENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO - NGARA

    May 16, 2025
  • KIKAO KAZI CHA UTEKELEZAJI WA MRADI WA AFUA ZA LISHE WA KILIMO CHA MAHINDI CHAFANYIKA - NGARA

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa