- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara hadi kufikia Machi 31, 2018, ilipokea shilingi bilioni 23,343,040,898.46, na kutumia shilingi bilioni 23,286,911,246.00/=, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo robo ya tatu 2017/2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama, amesema haya wakati wa Baraza la waheshimiwa Madiwani Mei 15, 2018, katika ukumbi wa Halmashauri.
Ndugu Bahama amefafanua kuwa katika kipindi cha 2017/2018, Halmashauri yake iliidhinishiwa na serikali kuu jumla ya shilingi 44,055,604,713.00; ambapo shilingi 28,615,809.00 zilitengwa kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi.
“Tulitengewa kiasi cha shilingi 1,165,473,000.00 kwa ajili ya matumizi mengineyo, shilingi 1,782,480,44.00 ziliidhinishwa kama mapato yatakayotokana na vyanzo vya Halmashauri, ambapo shilingi 12,492,185,457.00, ilitengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kutoka serikali kuu.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji.
Tangu Julai 2017 hadi Machi 31, 2018 Halmashauri ilipokea jumla ya shilingi 23,343,040,898.46, ambapo mchanganua wa fedha iliyopokelewa ameutaja kuwa shilingi 912,158,832.05, ilikusanywa kutoka katika vyanzo vya Halmashauri.
Jumla ya shilingi 17,087,159,760/= ilipokeliwa kutoka serikali kuu, kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi, ambapo kiasi cha shilingi 703,720,000/= kilipokelewa toka seririkali kuu, kwa ajili ya matumizi mengineyo, pamoja na shilingi 4,640,002,306.45, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Aidha, Halmashauri imetumia zaidi ya shilingi bilioni 23.2 kwajili ya kulipa mishahara ya watumishi, kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za afya, elimu na maji, pamoja na matumizi mengineyo.
Amesema kwamba Halmashauri yake imefikia wastani wa 35% ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali, na kwamba tangu Julai 2017 hadi Machi 31, 2018 Halmashauri yake, imetumia zaidi ya shilingi bilioni 4.6; fedha za Mfuko wa Maedeleo ya Jamii (TASAF III), HSBF, Mfuko wa Jimbo, ICAP/MHD na mfuko wa maji, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa