- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Madiwani Wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara umefanyika katika ukumbi mpya wa Halmashauri ya wilaya ulipo makao makuu Ngara mjini
Ambapo Mbunge Wa Jimbo la Ngara Mhe Doto Bahemu ameshiriki kikao cha Kwanza cha Baraza la Madiwani Wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kilichotanguliwana mchakato Wa kumpata Mwenyekiti Wa Halmashauri na Makamu wake ambapo ameungana na Madiwani wenzake kupiga Kura na Kumchagua Mwenyekiti Wa Halmashauri na Makamu wake. Uchaguzi huo umesimamiwa na Katibu Tawala Wilaya Bi Hatujuani Ally Lukari ambaye amewatangaza Mhe Wilbard Bambara kuwa Mwenyekiti Wa Halmashauri na Mhe Theofilda William kuwa Makamu Wa Mwenyekiti Baada ya Kura kuhesabiwa.
Naye Mhe Doto Bahemu Mbunge amewapongeza Sana Madiwani kwa kuaminiwa kwa Kishindo na wananchi katika Kata zao na kuwasisitiza kuhakikisha wanakuwa sehemu ya Kutoa majawabu katika changamoto zinazowakabili wananchi huku wakikumbuka kila wakati kuwa Maendeleo ya Wilaya ya Ngara na wananchi wake yako mikononi mwao na yeye kama Mbunge akaahidi Kutoa ushirikiano Wa Hali na Mali Kwao na kushirikiana nao bega kwa bega na Madiwani pamoja na Baraza ili kuhakikisha Maendeleo yanapatikana, changamoto za wananchi zinatatuliwa kwa wakati sambamba na Kuimarisha ustawi Wa Jimbo la Ngara
Mgeni rasmi katika katika mkutano huo alikuwa Mhe Col. Mathias Julius Kahabi Mkuu wa Wlaya ya Ngara ambapo alisisitiza
Waheshimiwa Madiwani na viongozi kuwasikiliza matakwa ya wananchi vijana wanawake na wazee na kutatua changamoto zao pia udhibiti wa magendo mipakani



Kazi na utu tunasonga mbele
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa