- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
28/03/2025
Kimefanyika kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa usimamizi wa Afua za Lishe robo ya Pili 2024/2025. Kikao kilichoongozwa na Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara ambaye alikuwa Mkiti na Bw Josephat Sangatati Kaimu Ded aliyekuwa katibu pamoja na Bw JawaduYusuph Kaimu Das
Kikao hicho kimehudhuriwa na Bi Vivian Maruhe kaimu Mkuu wa Idara ya utawala na usimamizi wa Raslimali watu , Emmanuel Msokwa Afisa lishe Wilaya, Maafisa Elimu Msingi na Sekondari pia Maafisa watendaji wa kata zote 22.
Akifungua kikao hicho Mhe Col Mathias J Kahabi - Dc Ngara aliwaagiza Maafisa watendaji wa kata kusimamia ipasavyo suala la lishe hasa kwa wanafunzi shule za Msingi na Sekondari alisisitiza wanafunzi wapate chakula shuleni ili waweze kufanya vizuri pia kwenye mitihani yao ya Mwisho kwa shule za Msingi na Sekondari .
Aidha Mhe Col Kahabi waliwataja Maafisa watendaji kata wanaofanya vizuri katika uchangiaji wa chakula Shuleni ambao ni Maafisa watendaji kata za Kirushya, Mugoma, kanazi, Rulenge na kabanga. Mhe Col kahabi alitoa nafasi kwa watendaji hao ili kutoa uzoefu jinsi walivyofanya vizuri na kufanikiwa katika kata zao.
Baada ya Mawasilisho ya kata hizo ilisisitizwa kata ziige mfano wa kata zilizofanya vizuri kwa kutoa chakula shuleni.
Mhe Col Mathias J Kahabi katika Picha ya pamoja na Bw Josephat Sangatati kaimu Ded ,Bw Jawadu Yusuph Kaimu Das na Maafisa watendaji kata za Rulenge. kabanga,kanazi ,mugoma na Kirusha
Maafisa watendaji katika kikao kazi cha tathmini ya mkataba wa usimamizi wa afua za lishe.
Afisa Lishe Bw Emmanuel Msoka na mwandishi wa vikao Halnashauri Bw Ally wakiwa kwenye kikao kazi
Ngara kazi inaendelea
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa