- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Kimefanyika kikao kazi cha tathmini ya Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) katika ukumbi wa Baba Askofu Uliopo Ngara Mjini.
Kikao cha Tathmini kilishirikisha maafisa Elimu Msingi utawala, Afisa Elimu Sekondari ,TSC, Uthibiti ubora wa shule na Utamaduni sanaa na Michezo.
Mgeni rasmi katika kikao hicho alikuwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Ndg. Solomon O kimilike.
Akitoa taarifa ya matokeo ya kumaliza Elimu ya Msingi ( PSLE) Mkuu wa idara ya Elimu Msingi Mwl James J Ling'hwa alisema zipo shule kumi 10 chini ya wanafunzi 40 Shule kumi (10) zaidi ya 40 , kata 3 zilizofanya vizuri , walimu wa masomo wanafunzi wao waliofanya vizuri .
Naye Afisa elimu taaluma Mwl Johnstone Adonise alizitaja shule 10 duni chini ya wanafunzi 40 na shule 10 duni ziadi ya 40.
Uwasilishaji wa mikakati ya kuinua taaluma shuleni kwa kila kata ulifanyika kwa kata zote 22 kuwasillisha ,baada ya zoezi hilo ndiyo yalipoingia majadiliano ya wote na kupata maazimio.
Aidha uwasilishaji wa ofisi za elimu utawala ulifanyika kwa Afisa Eliimu taaluma,Afisa Elimu maalumu,Afisaelimu watu wazima na Afisa elimu Takwimu na vifaa kuwasilisha mambo muhimu. Yanayohusu. Vitengo hivyo.
Pia Wenyekiti wa walimu wakuu, maafisa Elimu kata na Wakuu wa TSC ,Uthibiti ubora wa shule, Utamaduni/ michezo, Afisa Elimu secondary, na Mkuu Usalama wa Taifa( w) walimwasilisha Mgeni rasmi ambaye alikuwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Ndg. Solomon O kimilike alizipongeza shule zilizofanya vizuri ,kata na walimu. Wa Masomo. aliendelea kwa kumpongeza Mkuu wa idara ya Elimu Msingi Ndg James ling'hwa ,maafisa kwa kupanda asilimia tofauti na mwaka Jana 2023.
Mwisho Mgeni rasmi Ndg kimilike alikabidhi zawadi mbalimbali za washindi na watumishi wawili waliostaafu idara ya elimu
Picha za matukio mbalimbali ya kukabidhi zawadi zinafuata
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa