• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

KIWANDA CHA KISASA UCHENJUAJI NIKEL KUJENGWA TANZANIA

Wakati ilipowekwa: November 15th, 2023

● Zoezi la ulipaji fidia wananchi lazinduliwa  Wilayani Ngara,Kagera


● Kaya 1339 kulipwa fidia


● Wananchi 800 wameisha saini Mikataba ya Malipo

Imeelezwa kuwa takribani Kaya 1339 katika Wilaya ya Ngara wanatarajia kulipwa kiasi cha zaidi ya Shilingi bilioni 26 ikiwa ni sehemu ya fidia ya ardhi iliyotolewa kupisha mradi wa uchimbaji wa Madini Mkakati ya Nikeli katika eneo la  Bugarama Mkoani Kagera ambapo madini hayo ya Nikeli yatakayochimbwa yatachenjuliwa na kusafishwa hapa hapa nchini Tanzania kupitia kiwanda cha kisasa kitakachojengwa Kahama,Mkoani Shinyanga. 

Hayo yameelezwa leo Novemba 14 , 2023 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Ulipaji  fidia kwa wananchi waliopisha eneo la Mradi wa Uchimbaji wa Madini Mkakati ya Nikeli iliyofanyika katika viwanja vya Mgodi wa Kabanga Nikeli  Mkoani Kagera.

Waziri Mavunde ameeleza kuwa Mradi huu ni wa historia katika nchi zilizo Kusini Mwa Jangwa la Sahara ambao utatumia Teknolojia ya kisasa katika Uchimbaji na Uchenjuaji wa  Madini hayo nchini ambapo teknolojia itakayotumika ni ya kisasa ya hydro met.

Akielezea kuhusu Mipango ya Serikali katika uchimbaji wa Madini  Mkakati , Waziri Mavunde amebainisha  kuwa kwasasa Serikali inaandaa  mkakati wa usimamizi wa madini ya kimkakati na hasa katika kusimamia uongezewaji thamani wa madini hayo hapa hapa nchini. 

Sambamba na hapo Waziri Mavunde amesisitiza kuwa Serikali inachukua Mradi wa Tembo Nikeli kama sehemu ya Mradi wa kielelezo  kwa Miradi mingine ya Madini Mkakati  inayofuata.

Akitoa maelezo yake Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amesema kwamba serikali inatambua umuhimu wa mradi huu mkubwa wa kielezo na kwamba wizara ya ardhi itatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha kwamba zoezi la fidia linakamilika kwa wakati na wananchi wanapata haki yao kwa mujibu wa Sheria.

Wakitoa maelekezo ya Kamati za Bunge za Ardhi,Maliasili na Utalii na Nishati na Madini,Waheshimiwa Timothy Mnzava na Kirumbe Ng’enda wameitaka Kampuni ya Tembo Nikeli kuhakikisha inalipa fidia kwa wakati kwa wananchi wanaopisha mradi huo wa kimkakati.

Zoezi la uzinduzi wa ulipaji fidia lilishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwasa, Wajumbe wa Kamati za kuduma za Bunge zinazosimamia sekta za Ardhi na Madini,pamoja na Mbunge wa Ngara Mhe. Ndaisaba G.Ruhoro na wa viti maalum Mhe. Oliva Semguruka.

Aidha viongozi wengine walioshuhudia ni Mkuu wa Wilaya Mhe Kanali  Mathias Kahabi, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon Kimilike, kamati ya Usalama ,Wakuu wa Idara na Vitengo  Halmashauri pia viongozi  Mbalimbali wa chama na serikali.



Zoezi la ulipaji fidia wananchi  Waguswa wa Mradi wa Tembo nickel wazinduliwa wilayani Ngara Kagera

ngaradc.go.tz

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • DC NGARA MHE COL MATHIAS KAHABI AKUTANA NA BRIG GEN GABRIEL E. KWILIGWA - KAMANDA BRIGDE YA MAGHARIBI.

    May 16, 2025
  • MHE COL MATHIAS JULIUS KAHABI DC NGARA ASHIRIKI USAFI NA WANANCHI WA NAKATUNGA

    May 15, 2025
  • MWENYEKITI WA CCM AENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO - NGARA

    May 16, 2025
  • KIKAO KAZI CHA UTEKELEZAJI WA MRADI WA AFUA ZA LISHE WA KILIMO CHA MAHINDI CHAFANYIKA - NGARA

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa