- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA HABARI
9/12/2024
Yamefanyika Maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru kiwilaya Chuo cha Lemela kata ya Kanazi Wilayani Ngara.
Maadhimisho hayo yameshirikisha viongozi mbalimbali wa wilaya ambao ni Mkurugenzi Mtendaji wilaya Ndg Solomon Kimilike, katibu Tawala wilaya Bi Hatujuani Ally Lukari, kamati ya usalama wilaya, Wakuu wa idara na vitengo, watumishi, Wanachuo na Wananchi.
Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa Mhe Col Mathias Julius Kahabi Mkuu wa Wilaya Ngara.
Kauli Mbiu ikiwa :Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara " UONGOZI MADHUBUTI NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI NI MSINGI WA MAENDELEO YETU"
Mhe Col Kahabi alieleza mambo mbalimbali kwa kulinganisha kipindi cha uhuru na sasa kupitia sekta mbalimbali za Elimu, Afya, Barabaram Maji na Umeme. Mwisho Col Kahabi alimpongeza Dr Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta miradi mbalimbali katika wilaya ya Ngara.
Baada ya kumaliza Mhe Col Kahabi aliongoza zoezi la upandaji miti katika chuo cha maendeleo ya wananchi Lemela Ngara
Walifuata Ndg Solomon kimilike Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya, Bi Hatujuani Ally Likari Katibu Tawala Wilaya, Kamati ya Usalama Wilaya,Wakuu wa idara na vitengo , watumishi, wanachuo, na wananchi.
Adha pia lilifanyika zoezi la kufanya kufanya usafi wa mazingira kwa viongozi Mbalimbali na wananchi kushiriki zoezi la Usafi.
Mhe Col Mathias J Kahabi Mkuu wa wilaya Ngara akiongoza zoezi la upandaji miti chuo cha maendeleo ya wananchi Lemela kata ya kanazi wilayani Ngara.
Col Kahabi mkuu wa wilaya Akipanda Mti.
Ndg Solomon O kimilike Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Ngara akipanda Mti.
Bi Hatujuan A Lukari Katibu Tawala wilaya akipanda Mti.
Kamanda wa TAKUKURU Wilaya Ndg Ally Mikidadi akipanda Miti.
Col Mathias Kahabi Mkuu wa wilaya Akiongoza zoezi la usafi akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya Ndg Solomon Kimilike katika maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Tanzania Bara.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa