- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa ameiagiza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ifanye uratibu wa madai ya vyombo vya habari, sambamba na kuweka mfumo endelevu wa kutatua changamoto hiyo pamoja na changamoto nyingine za wanahabari.
“Taasisi zote za Serikali ziandae mpango wa kuhakikisha kuwa madai yote halali yanawekewa utaratibu maalum wa kuyalipa kwa sababu kuacha kulipa madeni haya ni kudhoofisha uchumi wa vyombo vya Habari".
Ameyasema hayo leo Novemba 13, 2023 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Saba wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) katika Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi.
Amewasisitiza wanahabari wote wafanye kazi kwa kufuata sheria za nchi na watambue mazingira ya kazi na kuweka tahadhari zote.
Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwataka Wanahabari wahakikishe wananchi wanapata habari zilizo sahihi na zinazohamasisha maendeleo. “Tunawahitaji sana hususani katika kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini".
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa