• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

MAJALIWA AZINDUA MITAMBO YA SHILINGI BILIONI 12.4 KWA AJILI YA WACHIMBAJI WADOGO

Wakati ilipowekwa: June 26th, 2025

 NGARA UPDATES

  • Ni kwa ajili ya uchorongaji na utafiti wa madini.
  • Asema ni mwendelezo wa juhudi za Rais Dkt. Samia kuboresha shughuli za wachimbaji wadogo
  • Atoa wito kwa wachimbaji wadogo kuuza madini ndani ya nchi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua mitambo kumi ya uchorongaji na vifaa vya utafiti wa madini yenye thamani wa shilingi bilioni 12.41 kwa ajili ya wachimbaji wadogo ambayo itapunguza changamoto za wachimbaji wadogo ya kufanya uchimbaji bila kuwa na taarifa za kijiolojia.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo uliofanyika leo Jumanne (Juni 24, 2025) kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa hatua hiyo ni mwendelezo wa juhudi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha shughuli za wachimbaji wadogo wa madini na kuwawezesha kuongeza uzalishaji.

“Oktoba 2023 Rais Dkt. Samia, alizindua mitambo mitano ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo. Kutokana na wingi wa wachimbaji wadogo nchini na mwitikio chanya wa wachimbaji wadogo alielekeza Wizara ya Madini kuongeza mitambo mingine”

“Mitambo hiyo mitano imeshatoa huduma ya uchorongaji kwa wachimbaji 16 katika maeneo mbalimbali nchini na kuchoronga jumla ya mita 3,450.37”

Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kuongezeka kwa mitambo ya uchorongaji maalumu kwa wachimbaji wadogo kutaleta mageuzi na manufaa makubwa katika sekta madini. “Moja ya faida kubwa za mitambo hiyo, ni pamoja na kuongeza chachu ya ukuaji wa shughuli za wachimbaji wadogo nchini kwa kuwa itawawezesha upatikanaji wa taarifa za uhakika za jiolojia”

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wachimbaji wadogo kuendelea kuuza madini katika viwanda vya ndani vya kusafisha dhahabu ili kuendelea kuchochea ukuaji wa uchumi nchini. “Na wale ambao wanashughulika na usafishaji wa madini, nendeni mkauze kwenye masoko yetu 43 yaliyopo na vile vituo 109, hakikisheni mzunguko wa madini unaanza kunufaisha Taifa letu badala ya kutorosha madini, kama kweli wewe ni mzalendo wa Taifa hili, popote utakapozalisha madini nenda kwenye masoko ya ndani ya nchi.”

Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha unaoishia, Sekta ya Madini imefanikiwa kuchangia katika mfuko mkuu wa Serikali kiasi cha shilingi trilioni 1.01. “Pamoja na maboresho haya, kwasasa katika benki Kuu ya Tanzania inahifadhi ya tani 5.7 na kuifanya Tanzania kuwa ndani ya kumi bora ya nchi zenye hifadhi ya dhahabu Afrika”.

Aidha, ameongeza kuwa katika miaka miaka ya minne ya Rais Dkt. Samia madarakani, sekta ya madini imeshuhudiwa ikifanya mapinduzi makubwa ikiwemo kuongeza mchango wake katika pato la taifa ambapo mpaka sasa inachangia asilimia 10.1 kabla ya mwaka wa kimalengo kufika 

Naye, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), John Bina ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia kwa uamuzi wake wa kuamua kuisimamia sekta ya madini ikiwemo kuwawezesha wachimbaji wadogo nchini.

“Madini ni sayansi na madini ni biashara, kwa maboresho haya, sasa watanzania wanachagamkia fursa katika sekta ya madini, wachimbaji sasa wanatosha kuchimba, wachimbaji wadogo tupo pamoja na Serikali yetu, hakika imetuheshimisha.”

www.ngaradc.go.tz

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • MAJALIWA AZINDUA MITAMBO YA SHILINGI BILIONI 12.4 KWA AJILI YA WACHIMBAJI WADOGO

    June 26, 2025
  • MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA YAFANYIKA KITAIFA DODOMA

    June 17, 2025
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA UFUNGUZI WA DARAJA LA J.P MAGUFULI (KIGONGO - BUSISI)

    June 19, 2025
  • KAGERA YAINGIA ROBO FAINALI MICHEZO YA UMITASHUMTA

    June 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa