• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KAMPASI YA UDSM - KAGERA

Wakati ilipowekwa: December 17th, 2025

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametoa wito kwa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kuhakikisha Kampasi mpya ya Mkoa wa Kagera inakuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu, mahali ambapo vijana watawezeshwa kuibua mawazo mapya, kufanya ubunifu, na kutumia fursa za soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mkoa wa Kagera, inayojengwa katika Kijiji cha Itawa Wilayani Bukoba. Amesema, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kihakikishe kuwa mitaala itakayotumika katika kampasi hiyo inalenga moja kwa moja katika kuleta maendeleo ya jamii kwa kutoa zaidi elimu - ujuzi, yaani mafunzo ya amali, kwa kuwa Mkoa wa Kagera na kanda yote ya ziwa ina fursa nyingi za kiuchumi.

Aidha, Makamu wa Rais amesema, kwa kuwa Mkoa wa Kagera unapakana na nchi jirani kadhaa, uwepo wa Kampasi hiyo utatoa fursa na kuvutia vijana katika nchi hizo kuja kujipatia maarifa muhimu. Amesisitiza Kampasi hiyo iwe ni mahali pa kukuza mtangamano wa Afrika Mashariki na kuendeleza umajumui wa Afrika ambao umekuwa msukumo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Vilevile, amesema ni tumaini kuwa, kupitia kampasi hiyo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitatoa mchango mkubwa katika kuendeleza maarifa katika ujasiriamali, kukuza ujuzi wa masoko, kuchochea biashara za mpakani, na kujenga uwezo wa vijana kuhimili ushindani katika soko la kikanda na kimataifa.

Halikadhalika, Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita imejizatiti kuendeleza jitihada za kuleta mabadiliko katika ngazi zote za elimu, hususan elimu ya juu kwa kuhakikisha kuwa wahitimu wanapata ujuzi, stadi na maarifa yanayoendana na soko la ajira.

Amesema, lengo kuu la Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (2025-2030) ni kukuza uchumi na kuimarisha ustawi wa wananchi, ambapo mojawapo ya njia ya kufikia azma hiyo ni kuongeza fursa ya elimu kwa vijana katika ngazi zote, ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu bila ada kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari.

Ameongeza kwamba, katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na hatua nyingine imefanya uamuzi wa kuhakikisha kila mkoa hapa nchini unakuwa na ama Chuo Kikuu au tawi la Chuo Kikuu.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amesisitiza umuhimu wa kuongezwa ardhi ya kutosha katika eneo hilo la ujenzi kwani lengo la kutoa ardhi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika miaka ijayo, ni kuiwezesha kampasi ili iweze kuwa Chuo Kikuu kinachojitegemea.

Amesema Kampasi hiyo inatarajiwa kuwa na miundombinu ya kisasa na kuzingatia viwango vya kimataifa. Pia amesema kipaumbele kinawekwa kuwa na mazingira rafiki yatakayoweza kukidhi mahitaji ya watu wote hususani wenye mahitaji maalum.

www.ngaradc.go.tz

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • DKT. MWIGULU ANAZUNGUMZA NA MACHINGA, MADEREVA PIKIPIKI NA BAJAJI

    January 08, 2026
  • SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA DED NGARA

    January 01, 2026
  • SALAMU KUELEKEA MWAKA MPYA 2026

    January 01, 2026
  • COL KAHABI DC NGARA AKAGUA MPAKA WA TANZANIA NA RWANDA UNAOTENGANISHWA NA MTO KAGERA

    December 24, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa