- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Miaka minne kasoro ya Uongozi wa serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais wetu mpendwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imekuwa na mafanikio makubwa sana katika sekta ya michezo, sekta ambayo imebeba matumaini makubwa ya vijana waliojiajiri kupitia vipaji mbalimbali walivyonavyo.
Si tu katika michezo iliyozoeleka na wengi, kama mpira wa miguu, kikapu na pete, bali Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amegusa pia michezo ya Masumbwi (Boxing) kwa kuendelea kusapoti vijana wanaoshiriki michezo hiyo.
Mwishoni mwa wiki hii, tumeshuhudia Mheshimiwa Rais akitoa motisha kwa mabondia walioshiriki kwenye BOXING SAFARI iliyofanyika katika Uwanja wa Zimbihile, wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera. Motisha ya Tsh. 10,000,000/= ilikabidhiwa na Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa kwa niaba ya Mh. Rais Samia kwa washindi 10 waliopatikana katika mapambano 10 yaliyopigwa siku hiyo.
Washiriki wa mapambano hayo na mashabiki wa Masumbwi mkoani Kagera, kwa pamoja wanasema upendo wa Rais Samia kwao wataulipa kwa kura za kishindo 2025 ili kazi iendelee kwa nguvu kubwa zaidi.
MICHEZO NI AJIRA, MICHEZO NI AFYA
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa