• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

MENEJIMENTI YA HALMASHAURI YAONGOZANA NA MKUU WA WILAYA KATIKA ZIARA YA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO MBALIMBALI KATA YA MURUKULAZO WILAYANI NGARA

Wakati ilipowekwa: April 6th, 2024

Menejimenti ya Halmashauri ikiongozwa na Mkurugenzi mtendaji Wilaya, wamefuata na Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Col Mathias J. Kahabi katika  ziara ya Kutembelea kijiji cha Murukulazo, Kata ya Murukulazo kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi  pia wakiwemo Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ngara Ndg. Jawadu Yusuph pamoja na Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndg Solomon Kimilike aliyewakilishwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Ndg Emmanuel Kulwa pamoja na Wakuu wa idara na vitengo Mbalimbali Halmashauri ya Ngara na Taasisi za Serikali. 

Katika mkutano huo wananchi waliuliza maswali, changamoto na KERO mbalimbali na *kujibiwa papo kwa papo na Wakuu wa Idara na Taasisi za Serikali* ambapo maswali changamoto na KERO zilijikita zaidi kwenye huduma mbalimbali za kijamii na miundombinu kama vile; Elimu, Afya, Barabara, Umeme, Maji, Ardhi, Kilimo na Mifugo.

Mhe Mkuu wa wilaya ameendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa elimu ili wananchi wazidi kuwapeleka watoto wao shule kwani watoto hao ndiyo kizazi kipya na tegemezi kwa Taifa siku za baadae.

Mhe Mkuu wa wilaya aliwaeleza Wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki vema katika dhana nzima ya Ulinzi shirikishi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kupunguza au kumaliza kabisa changamoto ndogo ndogo za Kiusalama zilizopo katika Kata na Vijiji vilivyopo mpakani ikiwemo Kata ya Murukulazo.

Mhe  Mkuu wa wilaya ametumia fursa hiyo kuwaonya Wananchi wachache wanaokaribisha wahamiaji haramu toka nchi jirani kwa mwanvuli wa kufanya kazi kama vibarua wa kulima mashamba alisema  tabia hiyo lazima iachwe mara moja  inahatarisha Usalama wa Mwananchi mmoja mmoja na Jamii kwa ujumla.

Pia amewataka Viongozi wa Kijiji cha Murukulazo kuwa na utaratibu ulipo kwa Mujibu wa taratibu na Sheria wa kusoma taarifa za mapato na matumizi kwa Wananchi kupitia Mkutano Mkuu wa Serikali ya Kijiji ambapo Wananchi wanaipata fursa ya kuuliza maswali na hoja mbalimbali kuhusiana na taarifa za miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya kijiji toka vyanzo mbalimbali vya mapato ama toka Serikali kuu, michango ya Wananchi nk.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Col Mathias Julius Kahabi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kuleta fedha za Miradi ya Maendeleo Wilayani Ngara.




ngaradc.go.tz

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • NGARA YAFANYA VIZURI MICHEZO YA SHULE ZA MSINGI UMITASHUMTA NGAZI YA MKOA

    May 30, 2025
  • MHE. COL MATHIAS KAHABI DC NGARA AKUTANA NA BALOZI WA RWANDA.

    May 29, 2025
  • NGARA YAENDELEA VIZURI NA MICHEZO YA SHULE ZA MSINGI UMITASHUMTA NGAZI YA MKOA.

    May 26, 2025
  • MADEREVA WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI ILI KUPUNGUZA AJALI - NGARA

    May 24, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa