- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
05/03/2025
Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi na Raslimali watu Bi. Jenifer Mapembe alianza ziara tarehe 04/03/2025 kwa kutembelea Hospitali ya Nyamiaga na kufanya kikao kazi na watumishi wa Hospitali hiyo.
Leo Tarehe 05/3/2025 Mkuu huyo wa Idara akiongozana na Ndg Rutakinikwa Paschal - Afisa utumishi walipokelewa na Katibu wa Hospitali ya Murgwanza Ndg Andrew Nziko na kaimu Mganga Mkuu.
Lengo la kikao kazi ikiwa ni kukumbushana Majukumu ya kazi na kujitambulisha , kufahamiana baada ya kuhamia wilaya ya Ngara.
Bi Jenifer Mapembe amefanya kikao kazi na Watumishi wa Hospitali teule ya Murgwanza akisisitiza mambo mbalimbali katika utumishi wa Umma ambayo aliyafafanua kama ifutavyo,
Kufuata sheria ,kanuni na taratibu,Maadili ya kazi ,Haki na wajibu,kutoa huduma bila upendeleo,kufanya kazi kwa uadilifu,kuwajibika kwa Umma kwa kuwahudumia vizuri na kuwahi kazini.
Aidha aliendelea kusisitiza matumizi sahihi ya taarifa kwenye taasisi,kutoa huduma nzuri (Custamer Care ) kwa Wananchi , Utunzaji siri kwa Wagonjwa na ofisi pamoja na Matumizi mazuri ya teknolojia.
Aliendelea kuwasisitiza watumishi kuhakikisha wanautumia vizuri mfumo wa upimaji utedaji kazi wa Serikali PEPMIS Kupendana na kushirikiana kazini . Mwisho aliwapongeza kwa kazi nzuri
Naye Katibu wa Hospitali hiyo amemshukuru Mkuu huyo wa idara kwa
Kuwatembelea na kuongea na watumishi ili kukumbushana mambo Mbalimbali ya kiutumishi.
Bi Jenifer Mapembe Mkuu wa idara ya utawala ,usimamizi na raslimali watu akiwa na Ndg Rutakinikwa Paschal na kaimu mganga mkuu hospital teule ya Murgwanza
Watumishi Hospital teule ya Murgwanza wakiwa kwenye kikao kazi cha Mkuu wa Idara ya utawala ,usimamizi na Raslimsli watu.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa