- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
03/05/2025
Mkuu wa Mkoa wa kagera Mhe Hajat Fatma Mwassa ameendekea na ziara kwa kutembelea ya kukagua Miradi Mbalimbali ya Maendeleo katika Wilaya ya Ngara.
Mhe Hajat Fatma Mwassa amefuatana na katibu Tawala Mkoa Kagera Ndg. Stivin M. Ndaki , Mhandisi wa Mkoa na Viongozi Wengine toka Mkoani.
Katika ziara hiyo Viongozi wa Ngara akiongoza Mhe Col Mathias Kahabi Mkuu wa Wilaya pia Ndg Somon kimilike Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya , kamati ya usalama na wataalam wa Halmashauri.
Mhe Hajat Fatma Mwassa ametembelea na kukagua miradi ifuatayo
Aidha Mhe Hajat Fatma Mwassa Amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Ngara kwa usimamizi mzuri wa miradi mikubwa na mizuri ya Maendeleo Aidha amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi za Miradi kwa wilaya ya Ngara pia Halmashauri zote za Mkoa wa kagera.
Mhandisi Magoli Meneja TARURA akitoa taarifa ya Mradi wa ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami kwa Mkuu wa Mkoa Wa kagera Mhe Hajat Fatma Mwassa . Barabara inayoitwa Magereza - Mukididili
Barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami
Ikiwasilishwa taarifa ya ujenzi wa shule ya mchepuo wa kiingereza inayojengwa kwa mapato ya Ndani
Mkurugenzi Mtendaji wilaya Ndg Solomon kimilike akimuongoza Mhe Hajat Fatma Mwassa kukagua Vyumba vya madarasa shule mpya ya mchepuo wa kiingereza.
Mhe Hajat Fatma Mwassa akiongea na Mhe Col Mathias J kahabi Mkuu wa wilaya pia Ndg Solomon kimilike Mkurugenzi Mtendaji Wilaya baada ya kumaliza kutembelea na kukagua shule ya mchepuo wa kiingereza
Mhe Hajat Fatma Abubakari Mwassa alipotembelea mradi wa ujenzi wa Soko la kimkakati Nzaza kabanga
Soko Mkakati la Nzaza kabanga mafundi wakiendelea na kazi
Mhe Hajat Fatma Mwassa Mkuu wa mkoa wa kagera akiangalia Daraja la kumwendo
Daraja la kumwendo hili ambalo litaondoa adha waliyokuwa wakipata wananchi kushindwa kuvuka wakati wa mvua.
Mhe Hajat Fatma Mwassa alipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la kufulia, Jengo la utawala na Jengo la Mionzi katika Hospitali ya Wilaya
Mhe Hajat Fatma Mwassa akipokea taarifa ya ujenzi wa Chuo cha Ngara Veta kinachojengwa Rulenge akiwa na Mhe Col Mathias J kahabi Dc Ngara
Chuo cha VETA NGARA Kinachojengwa Rulenge
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa