- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
01/05/2025
Maadhimisho ya Sherehe za wafanyakazi Mei Mosi kimkoa zimefanyika kwenye uwanja wa Posta ya Zamani Ngara Mjini.
Sherehe zilizoanza kwa maandamano ya watumishi kupitia vyama mbalimbali vya wafanyakazi ambapo maandamano yalipokelewa na Mgeni Rasmi Mhe Hajjat Fatma Abubakari Mwassa Mkuu wa Mkoa wa kagera.
Sherehe zilihudhuliwa na viongozi ngazi ya Mkoa akiwemo Katibu Tawala Mkoa wa kagera Ndg stivin Mashauri Ndaki, waheshimiwa Wakuu wa Wilaya zote, wakurugenzi watendaji Halmashauri/manspaa, Makatibu Tawala wilaya na maafisa utumishi ambapo sherehe hizo ziliambatana na burudani mbalimbali Ngoma, kwaya na muziki wa kizazi kipya.
Mhe Hajjat Fatma Mwassa baada ya hotuba yake Nzuri iliyoshangiliwa na wafanyakazi alimshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassani kwa miradi mbalimbali ya Maendeleo katika mkoa wa kagera.
Mhe Hajatt Fatma Abubakari Mwassa akiwasili uwanja wa Posta Ngara Mjini
Wafanyakazi wakiingia kwa Maandamano uwanja Posta Ngara Mjini
Mhe Hajat Fatma Abubakari Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Kikundi cha Ngoma Pamoja tunaweza wakitumbuiza katika maadhimisho ya sherehe ya wafanyakazi uwanja wa Posta Ngara Mjini
Mhe Hajat Fatma Mwassa akiongoa na wafanyakazi wote waliohudhulia kiwanja cha Posta Ngara Mjini
Wafanyakazi mbalimbali wakiwa katika maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi kimkoa zimefanyika wilaya ya Ngara
Wafanyakazi katika maadhimisho ya sherehe za Mei mosi
Mhe Hajjati Fatma A. Mwassa wakati wa utoaji Zawadi kwa wafanyakazi hodari akiwa na viomgozi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi na mhe Col Mathias J kahabi Mkuu wa wilaya ya Ngara
Viongozi wa madhebu ya Dini
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa