- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi leo tarehe 10 Januari, 2026, ameendelea kupokea mawasilisho mbalimbali ikiwa ni mwendelezo wa kupata uelewa wa kina na taswira ya jumla kuhusu majukumu yanayotekelezwa katika Vitengo, idara na programu za Wizara ya Afya kikao kinachofanyika jijini Dodoma katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete.
Katika kikao hicho, Dkt. Samizi anapokea mawasilisho kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NASHCoP), Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria pamoja na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP) ambapo ni programu na miradi inayofadhiliwa chini ya Mfuko wa Dunia (Global Fund).
Aidha, mawasilisho hayo yanahusu hali ya utekelezaji wa miradi, matumizi ya rasilimali, pamoja na mikakati ya kuimarisha ufanisi wa programu hizo katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi ili kuhakikisha malengo ya kitaifa ya kudhibiti UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu yanafikiwa kwa wakati.
Dkt. Samizi amesisitiza umuhimu wa kufanya tathmini ya kina ya utekelezaji wa programu na miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Dunia (Global Fund), ili kuhakikisha rasilimali zinazotolewa zinatumika kwa ufanisi, uwazi na kuleta matokeo yanayokusudiwa kwa wananchi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa