- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
30/05/2025
Timu ya Michezo ya Wilaya ya Ngara iliyoshiriki michezo ya UMITASHUMTA Ngazi ya Mkoa imeweza kushika nafasi ya tatu 3.katika ushindi wa Jumla Kwa michezo yote iliyoshindaniwa.
Mashindayo hayo yaliyofanyika chuo cha ualimu katoke Wilayani Muleba Mkoa wa Kagera.
Mgeni rasmi alikuwa Mhe Stephen M Ndaki Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, pia walihudhuria Kaimu Afisa elimu Mkoa Ndg Saimon Chibon, Mkiti wa maafisa elimu Ndg Julius Shula Afisa Michezo Mkoa Ndg Kepha Elias . Kaimu Maafisa Elimu msingi, maafisa michezo na utamaduni walimu wa michezo .ambapo halmashauri zote za Mkoa wa kagera zilishiriki jumla ya wanafunzi wanamichezo 790 wameshiriki michezo na kuchaguliwa wanafunzi 120 kuunda timu ya Mkoa
Michezo ambayo Ngara ilifanya vizuri ni
Jumla ya wanafunzi 18 kutoka Ngara na walimu 2 wamechaguliwa kuunda timu ya Mkoa ambayo imeanza kambi tangu tarehe 30/05/2025 kujiandaa na mashindano ya UMITASHUMTA Ngazi ya Taifa yatakayofanyika Mkoa wa Iringa tarehe 7/6/2025
Katibu Tawala Mkoa wa kagera Mhe Stephen M. Ndaki aliyeshika kikombe ili kumkabidhi kapteni wa timu ya Ngara baada ya kuwa Mabingwa wa mchezo wa Mpira wa kikapu (Basketball)
Wilaya ya Ngara walipopokea kikombe cha Mpira wa kikapu baada ya kuwa bingwa wa mchezo huo
Mwl Olipa kutoka Ngara mwalimu wa mchezo wa Goal ball mpira kengere kwa watoto wenye huoni hafifi wakipokea pongezi kwa kushika nafasi ya pili kimkoa kutoka kwa katibu Tawala Mkoa Ndg Stephen M Ndaki. Wakati wa kufunga michezo ya Umitashumta Mkoa
Katibu Tawala Mkoa Ndg Stephen M.Ndaki akiwa na kaimu Afisa Elimu mkoa Ndg Saimon Chibon, Mkiti wa Maafisa Elimu Ndg Julius Shula na Mkuu wa Chuo cha Ualimu Katoke
Afisa Michezo Mkoa wa kagera Ndg Kepha Elis akitoa alipotoa taarifa ya michezo Ngazi ya Mkoa
Ngara kazi inaendelea
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa