- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
Leo tarehe 10/10/2024, Kamanda William Solla OCD Ngara ameendelea na zoezi la Utoaji Elimu kwa Wananchi wa Wilaya ya Ngara kuhusu kujiepusha kujichukulia sheria mkononi na hivyo kupelekea matukio mbalimbali ya mauaji kwa jamii.
OCD kamanda William ameendelea kutoa Elimu hiyo kwa jamii katika Kata ya keza Tarafa ya Rulenge . Aidha katika zoezi hilo Elimu kubwa imetolewa kwa jamii kuhusu Jamii Kuacha Kujichukulia Sheria Mkononi, Kuthibiti Migogoro Ya Kifamilia Inayosababisha Mauaji, Kuacha Kunywa Pombe Masaa Yote Toka Asubuhi Hadi Jioni na Jamii Kutoa Taarifa Zenye Viashiria Vya Makosa Ya Jinai.
OCD kamanda William anaendelea na zoezi la kutoa katika Kata zote 22 za Wilaya ya Ngara na mpaka sasa tayari ameshatoa Elimu katika Kata za NTOBEYE, BUKIRIRO, MABAWE, BUGARAMA, MBUBA, MURUSAGAMBA, NYAKISASA , NYAMIAGA(KUMUYANGE) na KANAZI. Zoezi hilo ni endelevu ili kuhakikisha Matukio Wanapungua Kama Siyo Kumalizika/kuisha Kabisa
Aliyetoa Elimu hiyo kamanda SP William Sola OCD NGARA akiwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Afisa Tarafa Rulenge, Diwani kata ya keza, Watendaji kata na Vijiji.
KamandaWilliam Solla OCD Ngara akiendelea na vikao vya utoaji Elimu Kwa jamii.
Ngara Kazi inaendelea..
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa