- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara leo
Mkuu wa Mkoa wa kagera Hajatt Fatma Abubakari Mwassa amefanya ziara Wilayani Ngara.
Mhe Hajatt Fatma alikuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa wadau kujadili utekelezaji Mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi Wilayani Ngara .
Mkutano huo uliohudhuliwa na viongozi wa Chama na Serikali pia viongozi wa Madhehebu ya dini na Taasisi Kwa makundi Mbalimbali. Ambapo Taarifa iliwasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wilaya.
Aidha baada ya hotuba yake Mhe Hajatt Fatma Mwassa alifanya ziara Kutembelea Mradi wa ujenzi wa hospital ya Wilaya inayojengwa Mbuba Wilayani Ngara.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Hajatt Fatma Mwassa akiwa katika picha ya pamoja na Mhe Mkuu wa wilaya Col Mathias Kahabi ,Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon kimilike Mkiti wa CCM Cde Vitaris Ndailagije, Mkiti wa Halmashauri Mhe Wilbard Bambara katika Ukumbi wa St Francis Ngara Mjini.
Mhe Mkuu wa Mkoa katika picha ya pamoja na kamati ya usalama.
Mkuu wa Mkoa Mhe Hajatt Fatma Mwassa akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na vitengo Halmashauri ya wilaya.
Mkuu wa Mkoa Mhe Hajatt Fatma Mwassa akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon Kimilike Kutembelea Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Mbuba.
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Solomon Kimilike akitoa maelezo Kwa Mhe Mkuu wa Mkoa Hajatt Fatma Mwassa kwenye Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya iliyopo kata ya Mbuba.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa