- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATES
31/03/2025
Ndugu Waislam na wananchi wote wa Wilaya ya Ngara Kwa Muonekano wa Mwezi Mpya wa Shawari , Tayari Ramadhani kareem imeisha Mwenyezimungu mwingi wa Rehma mwenye kutoa Neema (SWA) Atujaalie TAWFEEQ baada ya kumaliza Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Aidha Mhe Col. Kahabi anawatakia Eid Al Fitri Njema Waislam wote kusherehekea kwa Amani ,upendo umoja na Mshikamano, Amesisitiza tujiepushe na mambo yote yanayoweza kuhatarisha usalama wetu.
Pia Amesema tuendelee kumuunga Mkono Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuilinda TUNU yetu Adhimu ya Amani tuliyonayo.
Alimalizia Mhe Col Kahabi kuwa Disco Toto ni Marufuku na wenye changamoto yoyote ya kiusalama wananchi Watoe taarifa kwa Vyombo vya ulinzi na Usalama haraka iwezekanavyo.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa