- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mhe Col Mathias Julius Kahabi, DC Ngara kwa niaba ya Kamati ya Ulinzi na Usalama (KU) Wilaya anawatakia Wananchi wote wa Wilaya ya Ngara Maandalizi mema ya Sikukuu za Mwisho wa Mwaka Christmas na Mwaka Mpya 2025.
Wananchi wote washerehekee Sikukuu hizi kwa amani na utulivu huku Vyombo vya Usalama Wilayani Ngara wakiwa wamejipanga vema kuimarisha hali ya Ulinzi na Usalama katika maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya hususan maeneo yote ya Mikesha ya Sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya ikiwemo Makanisani pamoja na Kumbi za starehe na burudani.
Mhe Col Mathias Kahabi anawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kipindi chote cha Sikukuu kwa kutoa taarifa za matukio yasiyokuwa ya kawaida na yanayoweza kuhatarisha Usalama wa raia na mali zao.
Aidha, anapenda kusisitiza kuwa Disco Toto ni marufuku kupigwa kwenye Kumbi za starehe na yeyote atakayekiuka maagizo haya hatua stahiki za Kisheria zitachukuliwa mara moja.
Inashauriwa kuwa watoto muda wote katika matembezi yao wakati wa Sikukuu wafuatane na mtu mzima anaweza, mzazi au mlezi ambaye atahusika kuilinda Usalama wao.
Vijana wa boda boda wanaagizwa kujiepusha na uendeshaji wa pikipiki usiozingatia Sheria za Usalama barabarani. Aidha, uchomaji wa matairi popote pale kama ishara ya kuuona Mwaka Mpya ni marufuku.
Kwa mara nyingine tena Mhe Col Mathias Julius Kahabi anawatakia Wananchi wote wa Ngara Christmas njema na Heri ya Mwaka Mpya 2025 kwa siku chache zilizobakia.
Ahsante sana - Mulakoze Cyane.
Ngara Kazi inaendelea
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa