• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

Simamieni Ubora wa Huduma Katika Hospitali Zetu; Mh. Ndugulile

Wakati ilipowekwa: July 31st, 2018

Wasimamizi wa vituo vya afya na hospitali katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kusimamia utoaji wa huduma bora ya afya, na kwamba vituo ambavyo havitakidhi vigezo, vitashushwa au kufungwa kabisa.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Faustine Ndugulile (MB), ameyasema hayo wakati akiongea kwa wakati tofauti na wafanyakazi wa hospitali za Nyamiaga na Murugwanza Julai 29, 2018.

Amesema lengo la ziara yake iliyoanza Julai 16, 2018, katika mikoa sita ya Mara, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Geta na kuhitimishwa mkoani Kagera, kuangalia shughuli mbalimbali, na kutunuku vyeti kwa vituo vya afya na watu waliofanyakazi vizuri.

“Tutaweka vigezo vya kuainisha ubora wa kituo cha afya; tukikuta kituo cha afya kimeshuka yaani hakina viwango, kama kilikuwa kituo cha afya kinakuwa zahanati; pia hospitali ya wilaya tunaweza tukaishusha au kuifunga kabisa ikiwa haina vigezo stahiki.” Alisema Mh. Nduglile.

Amesema wizara ina mpago wa kusajili na kuvipatia leseni vituo vya afya na hospitali zote za serikali na za binafsi, ikionekana kituo hakina vigezo, kitafungwa  na msimamizi itabidi aeleze ni kwa nini wananchi hawapati huduma.

Amefafanua kwamba kinachotakiwa ni uwajibikaji na usimamizi mzuri, na kuongeza kwamba ikiwa usimamizi utakuwa mzuri, mapungufu yataisha, na wananchi watapata huduma bora ya afya.

Wizara inalenga kuweka vigezo vya ubora wa utoaji huduma ya afya; kwa hiyo ni jukumu la kila msimamizi katika eneo lake, kuhakikisha kwamba anatimiza wajibu wake, ikishindikana itabidi kituo kifungwe.

Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Ngara bado haijapiga hatua stahiki, kwani tathimini inaonesha kwamba mwaka 2016, ni asilimia 2% tu ya vituo vya afya ndivyo vilikuwa na nyota tatu, na kwamba katika tathimini nyingine Halmashauri imepata 26% ambapo kiwango cha chini cha serikali ni 80%.

Amewataka watendaji kuongeza kasi katika kuwahamasisha akina mama wajawazito, kuhudhuria kliniki, pia wasisitize suala la lishe, kwa madai kwamba kiwango cha ubora wa huduma katika maeneo hayo bado ni cha chini ikilinganishwa na kile cha taifa.

Aidha, amewapongeza wafanyakazi wa hospitali teule ya Murugwanza, kwani hospitali hiyo kadili ya tathimini ya Julai 2018 wilayani Muleba ina nyota nne, na imeibuka ya kwanza katika mkoa wa Kagera.

Katika ziara hiyo Mh. Ndugulile ameambatana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Dr. Marco Mbata, aliyewasisitiza wafanyakazi katika vituo vyote vya afya na hospitali wilayani Ngara, kuondoa mapungufu aliyoyaona waziri, ili vituo vyote mwakani viwe na nyota tatu na kuendelea.

 

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • DC NGARA MHE COL MATHIAS KAHABI AKUTANA NA BRIG GEN GABRIEL E. KWILIGWA - KAMANDA BRIGDE YA MAGHARIBI.

    May 16, 2025
  • MHE COL MATHIAS JULIUS KAHABI DC NGARA ASHIRIKI USAFI NA WANANCHI WA NAKATUNGA

    May 15, 2025
  • MWENYEKITI WA CCM AENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO - NGARA

    May 16, 2025
  • KIKAO KAZI CHA UTEKELEZAJI WA MRADI WA AFUA ZA LISHE WA KILIMO CHA MAHINDI CHAFANYIKA - NGARA

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa