- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo Tarehe 09/01/2024 Meneja Mahusiano - Mradi wa Tembo Nickel Cde Moses Rusasa, Afisa wa Ulinzi na Usalama wa Mradi huo pamoja na Viongozi mbalimbali Toka Tembo Nickel, Wamefika Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ngara kwa Mhe Col Mathias Julius Kahabi kwa ajili ya kutoa taarifa ya Mradi ilipofikiwa ambapo zaidi ya Waguswa(PAPs) 220 wameshalipwa fidia zao na zoezi hilo linaendelea.
Aidha, Cde Rusasa amemweleza Mhe DC Kahabi kwamba mpaka sasa hakujaripotiwa changamoto kubwa kuhusiana na zoezi hilo la ulipaji fidia na Elimu inaendelea kutolewa kuhusu mipango na matumizi sahihi ya matumizi ya fedha nyingi zinazolipwa kwa Wananchi waguswa wa mradi huo.
Mhe Col Mathias Julius Kahabi ameendelea kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa maelekezo kuhusu ulipaji wa haraka wa fedha hatimaye kuanza uzalishaji Mradi huo mkubwa wa Kimkakati utakaonufaisha Wananchi wa Wilaya ya Ngara, Mkoa wa Kagera na Taifa kwa ujumla.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa