• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

VIONGOZI WA MIKOA NA WILAYA WAAGIZWA KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI MBIO ZA MWENGE

Wakati ilipowekwa: April 8th, 2025

HABARI LEO 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2025, ambazo zinalenga kuchochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuleta maendeleo nchini.

Ametoa agizo hilo akiwa katika Shule ya Msingi Ukombozi, Ikwiriri, kabla ya kumkaribisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa, Ismail Ussi, kuzungumza na wananchi waliokusanyika kushuhudia uraghabishaji wa falsafa ya Mwenge wa Uhuru uliofanywa na wanafunzi wa shule hiyo.

Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuwa atahakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu kwenye maeneo yote ambayo Mwenge wa Uhuru utapita kukagua miradi ya maendeleo na kuwaelekeza Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanahamasisha wananchi kwa nguvu zote kushiriki shughuli hizo muhimu.

“Mbio za Mwenge zinahamasisha maendeleo, na ndio maana zinaambatana na uzinduzi wa miradi ya kimkakati ya maendeleo. Ushiriki wa wananchi ni fursa muhimu ya kuwajengea uelewa katika usimamizi na utekelezaji wa miradi hiyo” amesema Waziri Mchengerwa.

Aidha, Waziri Mchengerwa amemweleza Kiongozi wa Mbio za Mwenge Taifa, kuwa Wilaya ya Rufiji imepiga hatua kubwa katika miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule, barabara, masoko, vituo vya afya na zahanati, miradi ambayo baadhi yake itakaguliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu.

Kwa upande wake,  Ismail Ussi amesema kila Mtanzania anapaswa kuienzi falsafa ya Baba wa Taifa, akisisitiza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendeleza falsafa hiyo kwa kumkabidhi jukumu la kuongoza Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, ambapo miradi ya maendeleo itakaguliwa na kuzinduliwa pale itakapobainika kutekelezwa kwa viwango stahiki.

www.ngaradc.go.tz

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI ROBO YA TATU 2024/2025 WAFANYIKA UKUMBI WA COMMUNITY CENTRE NGARA MJINI

    May 07, 2025
  • MKUU WA MKOA MHE HAJAT FATMA ABUBAKARI MWASSA AENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDEKEO WILAYA YA NGARA

    May 03, 2025
  • MHE HAJJAT FATMA MWASSA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO WILAYA YA NGARA

    May 02, 2025
  • MKUU WA MKOA MHE HAJAT FATMA MWASSA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA WAFANYAKAZI ZAFANA KIMKOA WILAYA YA NGARA

    May 01, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa