- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Wananchi wa Ngara Mjini Leo wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Ndg Solomon Kimilike kwa Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Serikali ya kiingereza inayojengwa Nakatunga Mamlaka ya Mji Mdogo wa Ngara Mjini.
Akiongea Ndg Jumaa Minani ambaye ni mkazi wa Kumzenga amesema Ngara inakuwa historia kuwa na shule ya kwanza ya serikali ya mchepuo wa kiingereza tu hivyo tunaishukuru Serikali ya Mama Samia .
Naye Bi Anna Mariam Mkazi wa Ngara Mjini amesema Shule hiyo tutapeleka watoto wetu kwani anaamini kuwa Ada aitakuwa sawa na Shule za Binafsi hivyo anaipongeza serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. DKT Samia Suruhu Hassan .
Ndg Samson Nyabenda Mkazi wa Ngara Mjini amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wilaya ,Mkiti wa Halmashauri na Mhe Mkuu wa wilaya kwa kuamua kuwajengea wananchi shule ya msingi ya kiingereza kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri.
Ngara kazi inaendelea
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa