• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

WAZIRI JAFO AWAPONGEZA WAKUU WA NCHI EAC KWA KULINDA NA KUHIFADHI MAZINGIRA

Wakati ilipowekwa: November 26th, 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amepongeza viongozi Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano huo hatua inayosaidia kuimarisha Maisha ya wananchi wa ukanda huo hususan kuhifadhi mazingira.

Ametoa pongezi hizo aliposhiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaojadili masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Usalama wa Chakula uliotanguliwa na Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Usalama wa Chakula, Ngurduto Mkoani Arusha Novemba 2023.

Amesema kama nchi tunajivunia kuwa na Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha uhusiano mzuri na Mataifa mengine ya Afrika Mashariki na dunia kwa ujumla.

“Tunashukuru tupo hapa Arusha tunakutana mawaziri na viongozi wakuu wa mataifa hayo hivyo, mkutano huu ni muhimu sana kwa kuwa unahusisha ajenda muhimu ya mazingira na ambayo ni muhimu kwa usalama wa chakula,” amesema Dkt. Jafo. 

Mkutano huo unajadili mada mbalimbali zikiwemo Maazimio ya Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Nairobi na uwiano wa athari zake kwa eneo la Jumuiya, 

Maazimio ya Mkutano wa Mifumo ya Usalama wa Chakula Kuhakikisha Usalama wa Chakula kupitia mikakati na mbinu mbalimbali za kurekebisha na Kuonesha Mafanikio ya Kilimo cha kisasa, kinachotokana na matumizi ya teknolojia na mbinu mbalimbali za ubunifu katika eneo hilo.

Mkutano huo wa Majadiliano ya Juu unatarajiwa kutoa na msimamo wa pamoja wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuelekea Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi unaotarajiwa kufanyika Dubai kuanzia Novemba 28, 2023.

Kauli mbiu ya Mkutano huo ni “Kuongeza ustahimilivu wa mabadiliko ya tabia nchi kwa usalama wa chakula na mazingira endelevu katika ukanda wa Afrika Mashariki".




ngaradc.go.tz

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • DC NGARA MHE COL MATHIAS KAHABI AKUTANA NA BRIG GEN GABRIEL E. KWILIGWA - KAMANDA BRIGDE YA MAGHARIBI.

    May 16, 2025
  • MHE COL MATHIAS JULIUS KAHABI DC NGARA ASHIRIKI USAFI NA WANANCHI WA NAKATUNGA

    May 15, 2025
  • MWENYEKITI WA CCM AENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO - NGARA

    May 16, 2025
  • KIKAO KAZI CHA UTEKELEZAJI WA MRADI WA AFUA ZA LISHE WA KILIMO CHA MAHINDI CHAFANYIKA - NGARA

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa