• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

WAZIRI MKUU MHE KASIMU MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS DKT SAMIA KWENYE MKUTANO WA DHARURA WA SADC

Wakati ilipowekwa: February 2nd, 2024

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amemwakilisha Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa dharura wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Mkutano huo uliofunguliwa na Rais wa Angola, Joao Manuel Lourenco ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, ulikuwa na ajenda moja tu ya kujadili kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika ukanda wa SADC.

Akizungumza kutoka ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma leo (Ijumaa, Februari 02, 2024), Waziri Mkuu Mhe Majaliwa amesema Tanzania inapendekeza kuwa ni vema Kanda ya SADC ikachukua hatua jumuishi kwa kuhusisha sekta zote mtambuka ikiwemo sekta za maji na mipango miji ili kuleta suluhisho la kudumu la kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu na magonjwa mengine ya mlipuko.

“Hii ni kwa kuzingatia kuwa jamii kwa ujumla na kila mwananchi ana jukumu la kuchukua tahadhari kwa kuhakikisha anazingatia kanuni za usafi (WASH) kwa manufaa binafsi, jamii na ukanda mzima.”

“Tunashauri nguvu kubwa ielekezwe katika kuboresha mifumo na upatikanaji wa maji safi na salama katika jamii zetu ili kuwa na matokeo chanya katika kudhibiti mlipuko huu.”

Mkutano huo ulihudhuliwa na Waziri wa Afya, Mhe Ummy Mwalimu; Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.

Mapema, akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa SADC, Rais Lourenco alisisitiza umuhimu wa nchi wanachama kuimarisha mawasiliano baina ya wataalamu wake ili kusaidiana kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo hasa kwenye maeneo ya mipakani.

Aidha, alisisitiza viongozi wa nchi wanachama waweke kipaumbele kwenye teknolojia mpya na tafiti ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko. “Ni lazima tuhakikishe mifumo yetu ya afya inaweza kukabili na changamoto hizi za magonjwa ya mlipuko.”

Marais walioshiriki mkutano huo ni Phillipe Nyusi (Msumbiji), Lazarus Chikwera (Malawi), Emmerson Mnangagwa (Zimbabwe), Haikande Hichelema (Zambia) Felix Tshisekedi (DRC). Wengine ni wawakilishi wa Wakuu wa Nchi kutoka Afrika Kusini, Lesotho, Eswatini, Seychelles na Madagascar.

ngaradc.go.tz

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI ROBO YA TATU 2024/2025 WAFANYIKA UKUMBI WA COMMUNITY CENTRE NGARA MJINI

    May 07, 2025
  • MKUU WA MKOA MHE HAJAT FATMA ABUBAKARI MWASSA AENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDEKEO WILAYA YA NGARA

    May 03, 2025
  • MHE HAJJAT FATMA MWASSA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO WILAYA YA NGARA

    May 02, 2025
  • MKUU WA MKOA MHE HAJAT FATMA MWASSA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA WAFANYAKAZI ZAFANA KIMKOA WILAYA YA NGARA

    May 01, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa