• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

WAZIRI MKUU: SERIKALI YATENGA SHILINGI BILIONI 43 KUIMARISHA MICHEZO SHULENI

Wakati ilipowekwa: June 9th, 2025

NGARA UPDATES

▪️Azindua mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA Iringa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga Sh. Bilioni 43 ili kuimarisha michezo katika shule mbalimbali nchini na kati ya hizo, Sh. Bilioni 32 ni kwa ajili ya kuimarisha Chuo cha Michezo Malya.

Amesema shilingi Bilioni 11 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kuboresha miundombinu ya michezo katika shule za sekondari 10 ambazo ni miongoni mwa shule teule 56 za michezo nchini.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Juni 9, 2025) wakati akifungua mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari Tanzania (UMITASHUMTA na UMISSETA) kwenye viwanja vya Kichangani vilivyoko Kihesa, mkoani Iringa.

Akielezea mikakati ya Serikali ya kuendeleza michezo na sanaa nchini, Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuimarisha Chuo cha Michezo Malya ili kiendelee kutoa mafunzo kwa kuzingatia utaalam na kuimarisha ufundishaji wa masomo ya michezo shuleni.  

“Chuo hiki kikikamilika kitawanufaisha wanafunzi wanamichezo wanaoonesha vipaji katika mashindano haya,” amesema na kuongeza kuwa mpango huo unatekelezwa kwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya michezo na sanaa nchini kwa ajili ya kuandaa wataalam na wanamichezo mahiri.

Amesema Serikali imeendelea kuimarisha michezo katika ngazi zote za elimu ikiwemo kuratibu mashindano ya michezo ya Umoja wa Michezo na Taaluma katika shule za msingi, sekondari na vyuo ili kuibua vipaji vya michezo kuanzia ngazi za chini sambamba na kuanzisha shule za akademia za michezo.

Kuhusu mafunzo kwa walimu wa michezo, Waziri Mkuu amezitaka Halmashauri zote nchini zihakikishe walimu mbalimbali wanahudhuria mafunzo ya michezo katika vyuo mbalimbali ikiwemo Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya ili kupunguza uhaba wa watalaamu wa michezo katika shule mbalimbali na nchini kwa ujumla.

“Wapelekeni walimu katika vyuo vya taaluma kama Malya, Butimba na wale wanaopata sifa za kwenda vyuo vikuu waende wakaimarishe utaalamu wao, ili waalimu hawa wanapopewa timu basi tunakuwa na timu zenye uhakika kwamba zimefundishwa na walimu wenye uwezo ulioimarika.

Aidha ameitaka Wizara ya Elimu na Ofisi ya Rais TAMISEMI waimarishe usimamizi ili ratiba za shule zote ziwe na vipindi vya michezo na wahakikishe vipindi hivyo vinatumika kikamilifu.

Akielezea manufaa ya mashindano hayo ambayo yameiwezesha nchi kupata wachezaji wanaofuzu kucheza soka la kulipwa kwenye viwango vya kimataifa, Waziri Mkuu amewataka wanafunzi wanaoshiriki mashindano hayo waongezee bidii ili waweze kuibuka kidedea. Amewataja baadhi wa wanamichezo waliofuzu kuwa ni Mbwana Samatta (Ugiriki), Simon Msuva (Iraq), Novatus Miroshi (Uturuki), Kelvin John (Denmark), Abdi Banda (Afrika Kusini), Adi Yusufu (Uingereza) na Himid Mao (Misri).

Mapema, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi alisema mafanikio yanayoendelea kuonekana kwenye sekta ya michezo nchini, ni ushahidi tosha jinsi Serikali ya awamu ya sita ilivyodhamiria kukuza sekta hiyo.

Amesema Serikali imeendelea na ujenzi na ukarabati wa viwanja mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya michuano ya CHAN 2025 inayotarajiwa kuanza Agosti 2, mwaka huu. “Serikali inaendelea na ujenzi wa viwanja vya kisasa katika Jiji la Arusha na Jiji la Dodoma. Pia inafanya ukarabati wa viwanja vya mazoezi katika Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Arusha na inaendelea pia na ukarabati wa viwanja vya Benjamin na Uhuru jijini Dar es Salaam."

Naye, Naibu Waziri wa TAMISEMI (Elimu), Zainab Katimba alisema mwaka huu Serikali imetoa sh. Bilioni 2.4 ili kufanikisha mashindano hayo ya UMISSETA NA UMITASHUMTA.

Alisema katika kuboresha shule 26 za amali nchi nzima, Serikali imeanza na mikoa 10 na kwa mkoa wa Iringa, shule za sekondari za Iringa Girls’ na Lugalo zimepatiwa sh. milioni 450 ili kukamilisha ukarabati wa viwanja vya michezo.




Picha ya hiyo story ya ufunguzi michezo

www.ngaradc.go.tz

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • MAJALIWA AZINDUA MITAMBO YA SHILINGI BILIONI 12.4 KWA AJILI YA WACHIMBAJI WADOGO

    June 26, 2025
  • MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA YAFANYIKA KITAIFA DODOMA

    June 17, 2025
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA UFUNGUZI WA DARAJA LA J.P MAGUFULI (KIGONGO - BUSISI)

    June 19, 2025
  • KAGERA YAINGIA ROBO FAINALI MICHEZO YA UMITASHUMTA

    June 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa