- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara kwakushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Solomone Kimilike pamoja na wakuu wa Idara walizindua rasmi Mpango wa kutembelea Wananchi vijijini kufanya mikutano maalum ya kusikiliza kero,changamoto na kuzitafutia ufumbuzi
Ziara ya kwanza imefanyika katika Kijiji cha Mukalinzi kata ya Muganza, na imeonekana kuvuta hisia za wananchi kwakufurahia kuwaona Viongozi hao wa Wilaya wakifika vijijini na kuzungumza nao.
Kupitia mkutano huo wananchi walipata nafasi ya kuuliza maswali ambayo yalijibiwa na Wataalamu wa Halmashauri na Serikali kuu hasa NIDA,UMEME,MAJI,ARDHI,BIASHARA,TASAF,KILIMO NA MIFUGO pamoja na kupata taarifa mbali mbali kutoka kwa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi.
Kwa mpango huo wa ziara Vijijini kuwasikiliza Wananchi,kutatua changamoto na Kero zinazowakabili tunatoa pongezi. Hakika ile dhaa ya Utawala Bora sasa inaonekana.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa